Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diamond Platnumz anavyoendela kuitawala dunia ya muziki mwaka 2026

DIAMOND Pict

Muktasari:

  • Mwaka huu, wakati mkewe Zuchu akiendelea na malezi ya mtoto wao, mumewe ameendelea kukusanya kijiji kutokana na ziara yake ya kimuziki inayojulikana kama Retro Tour na tayari amepiga shoo katika nchi za Uganda na Rwanda.

KILA mwaka msanii supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amekuwa kionyesha ubora wake katika sanaa hiyo, huku mwaka huu 2026 akifanya makubwa hasa katika shoo zake.

Baada ya kujijengea jina ndani na nje ya nchi, Diamond ameendelea kuwa kipenzi cha mashabiki kila anakokwenda kutokana na shoo zake anazopiga akiwa mmoja wa wasanii wakubwa Afrika na wenye mafanikio makubwa.

Mwaka huu, wakati mkewe Zuchu akiendelea na malezi ya mtoto wao, mumewe ameendelea kukusanya kijiji kutokana na ziara yake ya kimuziki inayojulikana kama Retro Tour na tayari amepiga shoo katika nchi za Uganda na Rwanda.

Kwa sasa Mondi sio msanii anayetegemea wimbo mmoja au mbili kupiga shoo, ana hazina ya nyimbo zinazowapagawisha mashabiki wa zamani alivyoanza na hawa wa kizazi kipya. Kwa kifupi, amepiga shoo hizo akilenga mashabiki wote kwa kuchanganya nyimbo za zamani na za sasa.


DIAMO 01

SHOO YA UGANDA

Miongoni mwa shoo muhimu alizofanya mwaka huu ni ile ya Uganda na alitumbuiza Viwanja vya kriketi vya Lugogo 'Cricket Oval', vilivyopo jijini Kampala, Juni 5. Shoo hiyo ilimpa nafasi ya kukutana tena na mashabiki wake wa nchi hiyo ambao wamekuwa wakimuunga mkono kwa miaka mingi na ilikesha hadi alfajiri ya Juni 6.


DIAMO 02

AFUNIKA KIGALI

Kama kuna shoo iliyoonyesha ukubwa wa Diamond mwaka huu, basi ni ile ya Kigali, Rwanda, iliyofanyika Agosti 29, baada ya takribani miaka mitatu bila kufanya shoo kubwa nchini humo.

Katika shoo hiyo, Diamond alirejea kwenye Ukumbi wa BK 'BK Arena' akiwa sambamba na wasanii kama Bruce Melodie, Ish Kevin na Nel Ngabo kuonyesha uzoefu wake jukwaani.

Alipanda jukwaani kuanzia saa 12:42 jioni na alianza kwa kuimba wimbo wa 'Komasava' uliowapagawisha mashabiki kabla ya kuteremsha nyimbo 25 mfululizo, huku akiwapa mashabiki nafasi ya kuimba pamoja naye na kucheza.

Kilichovutia ni jinsi alivyolitawala jukwaa na kuliongoza anavyotaka huku akiwasiliana na mashabiki na kuwapa nafasi ya kuimba na kutumia dansi pamoja na timu yake kuongeza nguvu ya shoo.


DIAMO 03

NYIMBO ZA ZAMANI ZATIKISA

Katika shoo hiyo, aliimba nyimbo zake za zamani ukiwamo wa 'Marry You', aliomshirikisha Ne-Yo, pamoja na 'Why', alioimba na The Ben ambaye hakufika jukwaani kutokana na kuwa na shoo nyingine Uganda. Diamond aliwambia mashabiki alitamani kufanya naye wimbo huo jukwaani, lakini akalazimika kuendelea bila mshirika wake.

Nyimbo hizo za miaka ya nyuma zilikuwa ni ujumbe kwa mashabiki, wasimkumbuke Diamond wa sasa kwani safari yake kimuziki ilikuwa ndefu hadi kufika aliko.


DIAMO 04

SAA MOJA YA NGUVU

Kutokana na kanuni za burudani nchini huko, muziki ulitakiwa kuzimwa saa 2 usiku, lakini hilo halikumfanya Mondi kutumbuiza kinyonge na kwa saa 1:17 alizotumia zilitosha kuweka heshima yake Kigali, akionyesha uwezo wake wa kufanya shoo kwa muda mrefu bila kuchoka akiimba zaidi ya nyimbo 25.


DIAMO 05

BRANDI INAZIDI KUPEPEA

Kwa mtazamo wa kibiashara, ziara hii pia inaonyesha mabadiliko katika namna Diamond anavyouza brand yake. Hatumii tena jina la wimbo mmoja au albamu moja kama kivutio kikuu bali anauza historia ya muziki wake.

Kutokana na kuanza muziki muda mrefu, anawakutanisha mashabiki wa nyimbo za zamani na wa kizazi kipya na hivyo kuendelea kujiongezea umaarufu kila anakokwenda.


DIAMO 06

ZIARA INAENDELEA

Safari bado haijaisha. Baada ya vituo vya Afrika, Diamond ana ratiba ya Australia na Oktoba 10, atapiga shoo jijini Perth na Melbourne Oktoba 11 na matarajio ya huko ni makubwa zaidi kwani tayari ameshajitengenezea jina duniani.