Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diamond ageuka mtaalamu wa taarabu

DIAMOND Pict

Muktasari:

  • Mwanaspoti limemshuhudia Diamond alivyokuwa akifuatilia kila wimbo uliokuwa ukipigwa katika sherehe hiyo iliyofanyika Madale jijini Dar es Salaam, huku nyimbo za taarabu zilipoanza kusikika akionekana kuzijua na kuimba pamoja na muziki uliokuwa ukiendelea.

DIAMOND Platnumz ameonyesha kuwa taarabu si muziki wa kusikiliza tu kwake, baada ya kutawala sehemu ya burudani kwenye Henna Night ya Zuchu, akifuatisha nyimbo za taarabu, kuimba na kucheza huku akiwa karibu na mpenzi wake huyo.

Mwanaspoti limemshuhudia Diamond alivyokuwa akifuatilia kila wimbo uliokuwa ukipigwa katika sherehe hiyo iliyofanyika Madale jijini Dar es Salaam, huku nyimbo za taarabu zilipoanza kusikika akionekana kuzijua na kuimba pamoja na muziki uliokuwa ukiendelea.

Diamond hakuishia kwenye kuimba pekee, bali alionekana kucheza kwa kufuata midundo hiyo, huku wageni waliokuwa karibu naye wakipata burudani ya ziada kumuona msanii huyo wa Bongo Fleva akifurahia taarabu kwa namna ambayo huenda si kila siku mashabiki wake humuona.

Lakini burudani hiyo ilipata moto zaidi baada ya kupigwa wimbo “Huyu ni Wangu” wa mwanamuziki wa taarabu Abdul Misambano kutoka TOT. Diamond alionekana kumchukua Zuchu, akambeba huku akimkumbatia na kumbusu, akifurahia wimbo huo pamoja naye.

Katika hali hiyo ya furaha, Diamond alisikika akisema kuwa Zuchu ni wake, huku akiendelea kumbeba na kumkumbatia. 
Tukio hilo likawa miongoni mwa yaliyovuta macho zaidi kwenye usiku huo kutokana na namna wawili hao walivyojibu muziki huo wa mapenzi.

Nyimbo za taarabu ziliendelea kutawala burudani, huku Diamond na Zuchu wakionekana kuufurahia muziki huo bila kujisitiri. Wimbo mmoja baada ya mwingine uliendelea kuwafanya wageni kusimama, kucheza na kuimba, na Diamond naye akawa sehemu ya burudani hiyo.

Kwa kifupi, kama kuna mtu ambaye alionyesha kuwa Henna Night ya Zuchu haikuwa usiku wa kukaa na kutazama tu, basi alikuwa Diamond kwani aliimba taarabu, akacheza, akambeba Zuchu, akambusu na kusema ni wa kwake.