Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diamond afafanua ishu ya kuoa mke wa pili

DIAMOND Pict

Muktasari:

  • Mkali huyo jana aliachia kibao kipya cha mapenzi kiitwacho Msumari, ambacho hadi sasa kwenye mtandao wa YouTube kimepata watazamaji zaidi ya laki nane na kuongoza kwa namba moja katika chati za mtandao huo.

SUPASTAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul maarufu Diamond Platnumz amefafanua ishu ya kuoa mke wa pili, akisema hiyo ni kazi yake mpya.

Mkali huyo jana aliachia kibao kipya cha mapenzi kiitwacho Msumari, ambacho hadi sasa kwenye mtandao wa YouTube kimepata watazamaji zaidi ya laki nane na kuongoza kwa namba moja katika chati za mtandao huo.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Diamond aliandika, anashangaa kuona kuna tetesi zinazosambaa kwamba ameongeza mke wa pili, ilhali tayari ameoa na ana mke wake.

“Naona kuna misumari inapigiliwa kuwa Simba kaongeza mke. Hapana jamani, sijaongeza. Msinipe ujasiri nisiokuwa nao, na clip nyingine inasambaa nikiwa katika gari na msichana, hiyo ni video yangu nyingine ambayo pia inatoka muda si mrefu. Huu mwezi ni wa Raha na Burudani tu. Mambo ya ugomvi na wife aku mie sitaki,” ameandika Diamond.

DIA 02

Mwanzoni mwa Mei ilielezwa, Diamond alimuoa msanii anayemsimamia Zuhura Othman Soud maarufu Zuchu, ndoa ambayo haikuwekwa wazi zaidi na ilihudhuriwa na watu wachache.

Hata hivyo, mara kadhaa Zuchu alipofanyiwa mahojiano alieleza ndoa yake na namna anavyowajibika akiwa kama msanii na pia majukumu yake mengine kama mke.

Hivi karibuni kumekuwa na tetesi mitandaoni kuwa Diamond ameoa mke wa pili, akitajwa mtangazaji wa Wasafi Aaliyah. Wengine waliamini kweli, huku baadhi wakichukulia kama sehemu ya kiki.

DIA 03
DIA 03

Baadhi ya mashabiki waliona ni kiki ambayo msanii huyo amekuwa akiitumia ili kuwapa watu sikio hasa anapotaka kutoa wimbo mpya au kusaini dili jipya.

Kabla ya kuwa na Zuchu, Diamond alishawahi kuwa na uhusiano na mastaa kama Wema Sepetu, Zari The Bosslady (aliyezaa naye watoto wawili), Hamisa Mobetto (mtoto mmoja) na Tanasha Donna (mtoto mmoja).