Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Circumference ya Bebe Cool yazidi kupasua anga

Bebe Pict
Bebe Pict

Muktasari:

  • Singo hiyo ambayo ameirekodi katika mfumo wa video, ni utayarisho wa ujio wa albamu mpya itakayokwenda kwa jina la ‘Break The Chains’ atakayoachia mapema Aprili, mwaka huu.

MKONGWE katika muziki wa Uganda, Bebe Cool anazidi kuchanja mbuga na kibao chake 'Circumference' alichoachia hivi karibuni.

Singo hiyo ambayo ameirekodi katika mfumo wa video, ni utayarisho wa ujio wa albamu mpya itakayokwenda kwa jina la ‘Break The Chains’ atakayoachia mapema Aprili, mwaka huu.

Kazi hiyo iliyorekodiwa katika vivutio mbalimbali Afrika Kusini imeongozwa na mwogozaji daraja la kwanza, Garrick Williams - itakupa raha ya kuufaidi uzuri wa mandhari za Afrika Kusini.

Akizungumzia video hiyo na matayarisho ya ujio wa albamu yake mpya, Bebe Cool alisema: "Ujio wa wimbo wangu wa Circumference ni mwanzo wa ukurasa wangu mpya katika safari ya muziki."

"Ninafurahi kuwapa mashabiki na dunia nzima ladha hii nzuri ya muziki mzuri."