Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TUONGEE KISHKAJI: Godzilla alikuwa anapigisha pindi wasanii wenzake

Muktasari:

  • Kila Wakati imeandikwa kiutuzima, mashairi yamenyooka, yametulia, yanatoa ujumbe bila kuhubiri yaani yanatoa ujumbe na burudani juu.

NINAPOONGELEA ngoma zangu bora za wakati wote lazima niitaje 'Kila Wakati' ya Godzilla featuring G Nako. Ile ngoma ilikuwa ya moto na inawezekana ndiyo ngoma ya kwanza ambayo Godzilla alianza kuitengeneza kwa kuandika mashairi kwani King wa Salasala alikuwa mbaya sana kwenye mitindo huru; ngoma zake nyingi zilizohiti zilikuwa ni freestyle.

Kila Wakati imeandikwa kiutuzima, mashairi yamenyooka, yametulia, yanatoa ujumbe bila kuhubiri yaani yanatoa ujumbe na burudani juu.

Leo sio mara ya kwanza kupiga stori kuhusu ngoma ya Kila Wakati, mara ya mwisho wakati tunaichambua tuliangalia jinsi gani ngoma hiyo inawafundisha jambo waandishi wa habari, kwani ilipotoka, waandishi walidhani ni diss track kwa msanii fulani kwa sababu ukisiliza mashari yake yamekaa kama vijembe hivi.

Ngoma inaanza kwa mistari hii;

Kujua mziki homie that's not enough,

Ukishindwa rudi matawi ya chini omba upigwe tafu,

Desplicine kuwa nayo maintain yourself,

Lete kiburi upewe kiburi yaani u-burial-we safe.

Lakini 'Kila Wakati' ilitoka kipindi ambacho Godzilla amepungua uzito kwenye gemu, amepoteza ushawishi huku kukiwa na tetesi kwamba amekata ringi, anakula mihadarati na kushinda maskani Salasala, hana mpango. Huku wakati huo, Billnass akiwa anawika kwenye gemu akifananishwa na Godzilla kama sio kupewa jina la Godzilla mpya. Kwa hiyo hata Kila Wakati ilionekana ni kama dongo kwa Billnass.

Hata hivyo, tulivyoongelea Kila Wakati mara ya mwisho tulisema, vipi kama Kila Wakati ilikuwa ni dongo kutoka kwa Godzilla kwenda kwa Godzilla? Yaani vipi kama alijiandikia mwenyewe kujikumbusha kwamba mdogo wangu ulikuwa staa, ila sasa naona kama unafeli, hebu jaribu kurudi kwenye mstari.

Inawezekana ni kweli, inawezekana si kweli, lakini mbali na kwamba Kila wakati ilitufundisha jambo waandishi kwa mantiki hiyo, naamini kila wakati pia inawafundisha jambo wasanii.

Kwanini? Kwa sababu wasanii wakubwa wa filamu na muziki duniani hupenda kuandika nyimbo na filamu kuhusu uzoefu wa maisha yao. Na tukisema hivi hatuna maana kwamba wanaandika 'copy and paste' ya walichopitia, hapana. Bali wanaandika kulingana na hisia au nyakati za wanachopitia.

Kwa mfano, kama msanii anapitia furaha sana, basi ataandika ngoma kuhusu furaha, kulewa, kula bata na vitu kama hivyo, kama msanii anapitia nyakati ngumu za maisha labda kiuchumi, atatulia na kuandika filamu au ngoma kuhusu hali hiyo. Na kama msanii anapitia upendo mkubwa au pengine maumivu ya mapenzi ataandika kuhusu hicho. Ndiyo maana nadhani pengine Godzilla aliandika Kila Wakati kutokana na nyakati ngumu alizokuwa akipitia.

Sasa ukitazama ‘trend’ ya ngoma na filamu za wasanii wa Bongo unachokiona ni mapenzi tu. Kupenda, kupendwa, kuacha, kuachwa, kutendwa. Je ina maana wasanii wetu maisha yao yamejaa kitu kimoja tu? Mapenzi? Hakuna mambo mengine wanayopitia? Kama yapo kwanini wasiyatumie kama motisha ya kutengeneza kazi za sanaa ili kuondokana na kasumba ya kwamba sanaa ya kisasa imetawaliwa na mapenzi tu.

Na hivi vitu vinawezekana. Kama Mbaraka aliweza kutengeneza wimbo wa kuitwa Shida na bado wazee wa zamani wakaucheza disko, basi hata kina Marioo, Dimaond, Zuchu na Nandy wanaweza.