Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cecilia Godfrey ‘Ceccy’ kutoka Tanzania hadi Victoria’s Secret 

CECCILIA Pict

Muktasari:

  • Ceccy si jina linalotajwa tu kwenye ulimwengu wa mitindo, bali ni msichana anayebeba simulizi ya safari iliyoanzia nyumbani na kumfikisha mbali. Nyuma ya kila hatua kwenye maonyesho ya mitindo kuna changamoto, kujifunza na ujasiri uliomsaidia kuamini ndoto ya Mtanzania inaweza kufika dunia nzima.

ALIANZA na ndoto ambayo wengi wangeiona kuwa mbali kufikiwa, lakini Cecilia Godfrey maarufu kwa jina la Ceccy, hakuiangalia hivyo. Kutoka Tanzania, alichukua hatua moja baada ya nyingine hadi ndoto yake ya kuwa mwanamitindo ‘model’ ilipoanza kumfungulia milango nje ya nchi.

Ceccy si jina linalotajwa tu kwenye ulimwengu wa mitindo, bali ni msichana anayebeba simulizi ya safari iliyoanzia nyumbani na kumfikisha mbali. Nyuma ya kila hatua kwenye maonyesho ya mitindo kuna changamoto, kujifunza na ujasiri uliomsaidia kuamini ndoto ya Mtanzania inaweza kufika dunia nzima.

Safari hiyo sasa imemfikisha kwenye hatua nyingine kubwa kwani hivi sasa, Ceccy yupo kwenye mchakato wa kuwania nafasi ya kuwa mmoja wa malaika wa Victoria’s Secret.

Hata hivyo, bado hajafika mwisho wa safari hiyo, anaendelea kupambana kutimiza ndoto yake, huku mshindi akitarajiwa kutangazwa kwenye Victoria’s Secret Fashion Show 2026, Oktoba 18, 2026 jijini Los Angeles, Marekani.

Hatua hiyo tayari ni kubwa kwake, kwani inampa nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika moja ya majukwaa yanayojulikana zaidi kwenye ulimwengu wa mitindo.


CECCI 01

UZITO WA VICTORIA’S SECRET

Victoria’s Secret si jina geni kwenye ulimwengu wa mitindo kwani ni miaka mingi kampuni hiyo imejijengea umaarufu kutokana na bidhaa, kampeni na hasa Victoria’s Secret Fashion Show, ambayo imekuwa ikivuta macho ya mashabiki wa mitindo na burudani duniani.

Mwaka huu, kampuni hiyo imekuja na sura tofauti ya kusaka malaika mpya. Badala ya kutegemea majina makubwa pekee, ilifungua milango kwa watu wengi kushiriki kwenye shindano hilo. Zaidi ya watu 100,000 walijibu wito huo, kabla ya mchakato huo kuendelea chini ya mpango uliopewa jina la “Angels Among Us.”


CECCI 02

CECCY HAKUANZA LEO

Kabla ya Marekani na Victoria’s Secret, Ceccy tayari alikuwa ameshapita kwenye milango kadhaa ya shughuli za uanamitindo.

Safari yake ilianza nyumbani Tanzania na baadaye ikamfikisha kwenye mash indano na kazi za kimataifa.

Mwaka 2016 aliiwakilisha Tanzania katika Miss Teen Heritage International nchini Sri Lanka na kumaliza nafasi ya pili.

Baadaye akaendelea kusaka nafasi nje ya Tanzania, ikiwamo Dubai, kabla ya safari yake kumfikisha Marekani. Ceccy si msichana aliyelala Tanzania jana, akaamka leo akiwa kwenye reality show ya Victoria’s Secret kwani safari ya miaka kadhaa, nchi tofauti na majukwaa mbalimbali ambayo imekuwa msaada kwake kufika kwenye hatua nyingine.


CECCI 03

MAREKANI NI HATUA NYINGINE

Kuhamia Marekani kulimfungulia Ceccy ukurasa mpya katika safari yake ya uanamitindo, baada ya kupata uzoefu katika masoko mbalimbali ya nje, sasa anaendelea kujenga jina lake katika nchi ambayo ni miongoni mwa masoko makubwa ya mitindo duniani.

Hatua hiyo ndiyo iliyomfikisha kwenye “Angels Am ong Us”, na sasa kamera zinafuatilia safari yake mpaka alivofika sasa na wanamitindo wengine wanaowania nafasi ya kuwa Angel mpya wa Victoria’s Secret.

Mfululizo huo hauishii kwenye kinachoonekana jukwaani pekee. Unaonyesha safari nzima ya washiriki, kuanzia usaili na mchujo hadi hatua za mwisho za kuwania nafasi hiyo.

Kwa Ceccy, kila hatua ni nafasi nyingine ya kuonyesha uwezo wake na kuendelea kusogeza mbele ndoto iliyoanzia Tanzania.


CECCI 04

USHIRIKI WAKE KWENYE JUKWAA LA RICK ROSS

Safari ya Ceccy Marekani haikuishia kwenye maonyesho ya mitindo pekee, mwaka 2025 alipata nafasi ya kushiriki kama model kwenye uzinduzi wa bidhaa za msanii na mfanyabiashara Rick Ross, uliokwenda kwa jina la RR22.

Tukio hilo lililofanyika Florida Marekani, liliambatana na maonyesho ya mavazi yaliyowakutanisha watu kutoka kwenye ulimwengu wa mitindo na burudani. Ceccy alikuwa miongoni mwa wanamitindo waliopanda jukwaani kuonyesha mabegi.


CECCI 05

AINGIA KWENYE VIDEO YA LIL BABY

Safari yake Marekani imeanza pia kumfungulia milango kwenye ulimwengu wa muziki, ambako amepata nafasi ya kuonekana kwenye video ya “Mrs. Trendsetter” ya staa wa Marekani, Lil Baby iliyotoka mwaka 2025.

Ni hatua yake nyingine ya kujenga jina katika soko la burudani baada ya kuonekana kwenye jukwaa la uzinduzi wa mkusanyiko wa Rick Ross, sasa anaongeza uzoefu mwingine kupitia video hiyo, akizidi kujisogeza kwenye ulimwengu mpana wa fashion na burudani.


CECCI 06

CECCY NA LUKAMBA NJIA ZILITENGANA

Kabla ya safari yake ya uanamitindo kumfikisha Marekani, Ceccy alikuwa mke wa Lukamba, ambaye aliwahi kufanya kazi kama mpigapicha wa Diamond Platnumz. Uhusiano wao uliwahi kuwa sehemu ya maisha yake, kabla ya wawili hao kutengana.

Miaka mitatu imepita tangu Ceccy na Lukamba waachane, tangu hapo kila mmoja ameendelea na maisha yake.

Ceccy amekuwa akijikita zaidi kwenye uanamitindo, safari iliyomtoa Tanzania na kumfungulia milango ya kufanya kazi kwenye soko la kimataifa.