Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BURNA BOY: Dunia ya muziki inavyompa maisha

ATM Pict

Muktasari:

  • Burna ni miongoni mwa wasanii wa Afrika ambao wanatamba sana kwa sasa duniani hasa Ulaya na Amerika kutokana na nyimbo zake kupendwa sana huko.

LAGOS, NIGERIA: INAWEZEKAN jina la Damini Ebunoluwa Ogulu likawa geni masikioni mwako, lakini ukisikia Burna Boy hushtuki kama ni mfuatilia wa muziki.

Burna ni miongoni mwa wasanii wa Afrika ambao wanatamba sana kwa sasa duniani hasa Ulaya na Amerika kutokana na nyimbo zake kupendwa sana huko.

Mbali ya kutamba, staa huyu pia ni miongoni mwa wasanii wanaokula bata katika mataifa mbalimbali duniani kutokana na utajiri alioupata katika muziki.Hapa tumekuwekea mali anazomiliki na namna anavyoingiza pesa.

AT 01

ANAVYOPATA PESA

Kwa makadirio, hadi kufikia mwaka huu, Burna Boy ana utajiri wa takribani Dola 22 milioni, unatokana na mauzo ya nyimbo zake na shoo mbalimbali anazofanya, mikataba ya udhamini na uwekezaji sehemu mbalimbali.

Shughuli za muziki na shoo za kimataifa zinamwingizia kati ya Dola 10  hadi 17 milioni kwa mwaka.

Albamu zake za kimataifa na mikataba na majukwaa ya digital huongeza mamia ya maelfu ya dola kila mwezi na inakadiriwa ni zaidi ya Dola 5 milioni.

Ana mikataba ya udhamini na kampuni za Pepsi, Star Lager Beer, BoohooMan (UK), Fashion Collaboration, Apple Music, Spotify, Ciroc Vodka, Nike / Jordan Brand, MTN Nigeria Telecom.

katika mikataba hiyo ya udhamini kwa mwaka huingiza zaidi ya Dola 15 milioni.

AT 05

NYUMBA ANAZOMILIKI

Ana mjengo Lagos, Nigeri ambao una thamani ya Dola 1.5 milioni, jumba hilo la kifahari lina studio ya muziki, bwawa la kuogelea na bustani kubwa.

Pia ana nyumba London, England yenye thamani ya Dola 3.5 milioni, vilevile mjengo mwingine upo Ghana na Marekani. Thamani ya nyumba zake jumla ni takribani Dola 5 milioni.

AT 02

MSAADA KWA JAMII

Burna Boy hutoa msaada wa kijamii kwa njia mbalimbali, kwanza ni kupitia miradi ya elimu na misaada kwa watoto Afrika.

Aliwahi kutoa takribani Dola 200,000 kwa waathirika wa mafuriko Nigeria. Ana taasisi yake inayosaidia vijana katika muziki na sanaa.

AT 04

FAMILIA NA UHUSIANO

Mama yake, Bose Ogulu ni meneja wake wa muda mrefu, baba yake alikuwa mfanyabiashara na babu yake, Benson Idonije alikuwa meneja wa Fela Kuti. Familia yake ina historia ya muziki na biashara. Kwa sasa yupo katika mahusiano na mwanamuziki Chloe Bailey ambaye mara kadhaa wameonekana wote wakiwa pamoja Nigeria na sehemu mbalimbali.

AT 03

ANAVYOPONDA RAHA

Mara kwa mara huonekana kwenye ndege binafsi akisafiri kwenda Dubai, London na Marekani.

Mavazi yake si ya kitoto mara zote huonekana akivaa za brand maarufu kama Versace, Louis Vuitton, Gucci na Off-White.

Vilevile huonekana kwenye shehere mbalimbali za boti huko ufukweli ni miongoni mwa wasanii ambao huishi maisha ya starehe.