Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BONGO MUSICS FACTS: Hapa Nandy na Billnass, kule Jide na Mwana FA

Muktasari:

  • Akiwa miongoni mwa wasanii waliopitia Tanzania House of Talent (THT), ili kukinoa kibaji chake, kwa kipindi chote alichosikika amejenga himaya na sasa akiwa kama mmoja wa wasanii waliofanikiwa kisanaa na kiuchumi. Fahamu zaidi.

INGAWA hashiriki sana kuandika nyimbo zake, lakini hakuna ubishi kuwa Nandy ana sauti nzuri na melodi tamu. Vitu hivyo ndivyo vimemfanya kuendelea kuwepo masikioni mwa mashabiki kwa takribani miaka minane sasa.

Akiwa miongoni mwa wasanii waliopitia Tanzania House of Talent (THT), ili kukinoa kibaji chake, kwa kipindi chote alichosikika amejenga himaya na sasa akiwa kama mmoja wa wasanii waliofanikiwa kisanaa na kiuchumi. Fahamu zaidi.


1. Hadi sasa Nandy ameshinda mara nne Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2021 & 2023, mara moja The Orange Awards 2023 huku akitoa EP tatu Taste (2021), Maturity (2022) na Wanibariki (2021) pamoja na albamu moja, The African Princess (2018).

Kwa upande kimataifa ameshinda tuzo mbili za Africa Music Awards (AFRIMA) 2017 & 2020, AMI Awards Africa 2018, Africa Entertainment Awards USA (AEAUSA) 2021 na African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) 2021.


2. Nandy alisharekodi nyimbo mbili na Yemi Alade kutoka Nigeria, lakini hadi sasa hazijatoka. Walirekodi kabla hata ya Yemi Alade kusikika katika wimbo wa Harmonize ‘Show Me What You Got’ kutoka katika EP yake ya kwanza, Afro Bongo (2019).


3. Billnass ameshiriki katika kuandika wimbo wa Nandy, Dah! (2024) uliotoka kwa ajili ya harusi ya Haji Manara. Pia Nandy ameshiriki kuingiza sauti za chini katika wimbo wa Billnass, Sina Jambo (2017) uliotoka kabla ya wao kufanya kolabo yoyote.


4. Nandy ni msanii wa pili wa kike Bongo kufikisha wafuasi (subscribers) zaidi ya milioni moja YouTube baada ya Zuchu, ila kwa ujumla ni wa saba akiwa ametanguliwa na Diamond Platnumz, Harmonize, Rayvanny, Zuchu, Alikiba na Lava Lava.


5. Nandy alivutiwa na kipaji cha Yammi baada ya kumuona akiimba TikTok ndipo akamsanii katika lebo yake, The African Princess, akiwa kama msanii wa kwanza na kumtoa kupitia EP yake, Three Hearts (2023) yenye nyimbo tatu. Hata hivyo, Yammi sio msanii wa kwanza Bongo kutambulishwa na lebo yake kupitia EP, kuna Zuchu alitambulishwa na WCB Wasafi kupitia EP, I Am Zuchu (2020) na Mac Voice aliyetambulishwa na Next Level Music (NLM) kupitia EP, My Voice (2021).


6. Hadi sasa Jay Melody ndiye msanii aliyemwandikia Nandy nyimbo nyingi na zote zikafanya vizuri. Jay kamwandikia nyimbo nne ambazo ni Kivuruge (2017), Njiwa (2018) ft Willy Paul, Hallelujah (2019) ft Willy Paul na Do Me (2020) ft Billnass.


7. Wasanii wengine waliomwandikia Nandy ni pamoja na Billnass - Bugana (2019), New Couple (2021) na Dah! (2024). Pia kuna Marioo - Wasikundanganye (2017), Kusah - Nibakishie (2020) ft Alikiba na Lody Music - Napona (2022) ft Oxlade.


8. Huu ndio mwaka ambao Nandy ameshirikishwa zaidi na wasanii wenzake wa kike ndani ya Bongofleva. Amesikika katika wimbo wa Mimi Mars, Pole (2024), Yammi - Lonely (2024) na Maua Sama - Poa (2024).


9. Msanii wa kiume ambaye Nandy kashirikiana naye mara nyingi zaidi ni mumewe Billnass. Wawili hao wametoa pamoja nyimbo tano ambazo ni Bugana (2019), Do Me (2020), Party (2021), Bye (2022) na Totorimi (2024) unaofanya vizuri sasa.


10. Hiyo ni sawa na wasanii Mwana FA na Lady Jaydee ambao wamepiga kolabo tano pamoja ambazo ni Sitoamka (2002), Wanaume kama Mabinti (2003), Alikufa kwa Ngoma (2004), Hawajui (2005) na Msiache Kuongea (2009). Ikumbukwe pia Mwana FA ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Lady Jaydee walishirikishwa na Ngweah katika wimbo wake ‘Sikiliza’ kutoka katika albamu yake ya kwanza (A.K. A Mimi 2004) chini ya Bongo Records.