Isha Mashauzi awajibu mashabiki
Muktasari:
- Isha mashauzi hajatoa wimbo mpya kwa miezi kadhaa tofauti na alivyozoeleka kabla hajaingia kwenye biashara ya chakula na alikuwa ni mtu wa kutoa nyimbo kila wakati na mara ya mwisho ni Julai 2025.
Msanii wa muziki wa Taarabu, Isha Mashauzi amewajibu mashabiki zake wanaodai amewasaliti kuwapa burudani ya muziki na kuwa bize na biashara ya chakula.
Isha mashauzi hajatoa wimbo mpya kwa miezi kadhaa tofauti na alivyozoeleka kabla hajaingia kwenye biashara ya chakula na alikuwa ni mtu wa kutoa nyimbo kila wakati na mara ya mwisho ni Julai 2025.
Akizungumza na Mwanaspoti, Isha amesema mabadiliko aliyofanya ya kuongeza bishara ya chakula hayamaanishi kuwasahau mashabiki zake, bali ni sehemu ya kutafuta riziki na kuwasanua kuna nyimbo zipo tayari bado tu kuziachia.
“Mimi sipo kimya kwenye muziki na siyo nakuwa jikoni. Napata muda mwingi wa kuandaa kazi zangu za muziki na ziko tayari, bado tu kuziachia kwa mashabiki zangu, hivyo mimi si msaliti, naheshimu sana mashabiki zangu, unajua mashabiki ndio msingi wa kila kitu katika safari yangu ya muziki,” amesema Isha Mashauzi ambaye pia ni mkurugenzi wa Mashauzi Classic Modern Band.
Ametoa nyimbo kali kama 'Nani kama mama', 'Viwavi Jeshi' 'Nimpe Nani' na nyingine nyingi.