Bomu la Shaa likilipuka mtapoteana
MWANDISHI WETU HUTAMSIKIA Shaa kwa muda mfupi lakini akiibua bomu lake atakalolipua mtapoteana. Binti huyo mwenye mvuto Bongo yupo mafichoni akifanya mambo ya ukweli na akisoma nyendo za wapinzani wake akaibuka tu wamekwisha kimuziki. Msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Sarah Kaisi 'Shaa' amesema kwa sasa yupo chimbo akiandaa kazi zake mpya ambazo anazitoa baadaye mwaka huu ingawa ametajwa kushiriki katika tuzo za Channel O Music Awards miezi michache ijayo kupitia video yake ya 'Crazy' katika kipengele cha 'Most Gifted Afro-Pop Music Video'. "Baada ya kutoa Crazy kupitia audio na video, sijaishia hapo kwani kimya changu ni kutokana na kuisumbua akili yangu ili nifanye kazi nzuri zaidi ya hiyo ambayo wengi wataikubali. Video yangu ya Crazy imebahatika kupata nafasi kubwa sana katika tuzo mbalimbali, lakini nahitaji huu usiwe mwisho wangu, naandaa kazi zangu ambazo nitaziachia hivi punde" alifafanua.