Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BILLNASS: Namheshimu Nandy, watoto nane freshi

Muktasari:

  • Billnas ambaye anatamba na wimbo 'Magetoni' amekutana na mwandishi wa Dakika 5 Na... na kufunguka kuhusu maisha yake ya muziki na ndoa yake na Nandy na kuhusu watoto. Kwani ameachana na Amapiano?

WILLIAM Lyimo ndiye 'Billnass' kama hujui na kingine ambacho hujui ni maana ya jina hilo.

Billnass ambaye anatamba na wimbo 'Magetoni' amekutana na mwandishi wa Dakika 5 Na... na kufunguka kuhusu maisha yake ya muziki na ndoa yake na Nandy na kuhusu watoto. Kwani ameachana na Amapiano?


Mwanaspoti: Kwani Amapiano hailipi?

Billnass: Hapana sio Amapiano hailipi, bali nimeamua kurudi kuimba kwenye nyimbo zilizonitambulisha kwa mashabiki wangu na ambazo zimezaa jina la Billnass.

Mwanaspoti: Kwanza hapo hapo Billnass maana yake ni nini?

Billinass: Maana ya Billnas ni jina lililotokana na langu halisi la William Nicholaus, yaani William ni (Bill) na Nicholus (Nas).


Mwanaspoti: Wanamuziki wengi wanaogopa sana kuoa wanajua ndiyo mwisho wa muziki wao, unazungumziaje hilo?

Billnass: Kwangu sidhani kana kuna haja ya kuwa muoga kwenye hili, sababu hilo jambo ni wajibu kilitimiza, sasa hayo  mambo ya kuoa ndiyo mwisho wa muziki, sio kweli ni vile tu mtu atakavyojiwekea mikakati yake.


Mwanaspoti: Kila mwanamuziki huwa na mipango yake ya baadaye kwenye muziki wewe hili likoje?

Billnass: Ikifika muda wangu nitaachana na muziki na kufanya biashara.


Mwanaspoti: Wewe ni rafiki mkubwa sana wa Idrissa Sultan, lakini watu wakiona mnavyotaniana kwenye mitandao ya kijamii utasema ni maadui, hii imekaaje kwako?

Billnass: Mimi sio rafiki wa Idrissa, nawezaje kuwa na rafiki kama yule kichwa kibovu jamani (Kicheko), yule mie namuonagaonaga tu (kicheko).

Mwanaspoti: Kuna baadhi ya watu wanasema Nandy ni mkorofi hii ni kweli?

Billnass: Tatizo wanaosema hivyo hawajawahi kukaa naye na wengine hawamjui zaidi ya kumuona mitandaoni, ila ni kwamba Nandy ni mwanamke ambaye hapendi mambo ya ugomvi kabisa.


Mwanaspoti: Ushawahi kumpiga Nandy kwa kosa lolote lile?

Billnass: Sijawahi na hata sitawahi kumpiga Nandy na kitu ambacho nineumbwa ni kutokugombana na mwanamke au kumpiga mwanamke, nawaheshimu sana wanawake.


Mwanaspoti:  Mara nyingi tunaona uhusiano wa kimapenzi baina ya watu wanaofanya kazi moja ni ngumu hasa kwa upande wenu wanamuziki ni ngumu zaidi kudumu kwenye uhusiano unazungumziaje hilo?

Billinass: Kwa upande wangu au wetu ni ngumu hilo kutokea kabisa, tuna misingi mikubwa sana tumejiweke na kingine Nandy ni kama rafiki yangu, hivyo tunajuana na tunaweza kufanya mambo mengi bila tatizo.


Mwanaspoti: Ungependa kuzaa watoto wangapi na Nandy?

Billnass: Mimi napenda sana watoto na yeye anajua kabisa, tumekubaliana tuzae watoto nane alafu ndiyo atapumzika.

Mwanaspoti: Huwa unajisikiaje au kufanya nini Nandy akiandamwa na mashabiki au wasanii wenzake kwenye mitandao ya kijamii.

Billnass: Kila siku namwambia hauwezi kuwa na jina kubwa ushindwe kupitia mambo kama hayo, hivyo nampa moyo tu aendelee kupiga kazi.


Mwanaspoti: Ugomvi mwingi wa wapenzi unatokana na simu, kwa upande wako simu haijawahi kuleta shida kwenye uhusiano wenu?

Billnass: Hakuna kabisa na sisi kila mmoja anashika simu ya mwenzake muda wowote anaotaka, anajua namba yangu ya siri, najua yake ndiyo maisha yetu.


Mwanaspoti: Hivi karibuni Yanga unaionaje?

Billnass: Iko fresh tu, kwani kuna shida? Kufungwa ni kawaida katika mchezo ila sio kufungwa kwa kila mechi. Nina imani na timu yangu na suala la ubingwa liko pale pale. Yanga itawashangaza baadhi ya watu wanavyoifikiria kwa sasa. Ni kwa kocha na wachezaji kutokukata tamaa kutokana na maneno ya watu.