Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bagamoyo yageuka uwanja wa sanaa

BAG Pict

Muktasari:

  • Tamasha hilo lililoanza Oktoba 28, 2026, likitarajiwa kuhitimishwa Oktoba 31, 2026, limekusanya vikundi na wasanii kutoka maeneo mbalimbali nchini na nje ya Tanzania, huku majukwaa tofauti yakitumika kuonesha vipaji na utajiri wa sanaa na utamaduni.

NGOMA za asili, sarakasi, maigizo, muziki na ushairi ni miongoni mwa burudani zinazovuta hisia za washiriki katika Tamasha la 44 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, linaloendelea mjini Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.

Tamasha hilo lililoanza Oktoba 28, 2026, likitarajiwa kuhitimishwa Oktoba 31, 2026, limekusanya vikundi na wasanii kutoka maeneo mbalimbali nchini na nje ya Tanzania, huku majukwaa tofauti yakitumika kuonesha vipaji na utajiri wa sanaa na utamaduni.

Maonesho hayo yamegawanywa katika majukwaa mbalimbali, yakiwemo jukwaa kuu la nje, jukwaa la ndani na jukwaa la Mwembeni ambako pia kuna maonesho ya filamu.

BAG 01

Akizungumza na Mwanaspoti, Kaimu Mkuu wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo, Gabriel Kiiza, amesema historia ya tamasha hilo ilianza mwaka 2002 likiwa sehemu ya shughuli za wanachuo kuonesha fani mbalimbali wanazosomea.

Amesema kadiri miaka ilivyopita, tamasha hilo limeendelea kukua na kuwa jukwaa linalokutanisha wadau wa sanaa kutoka ndani na nje ya nchi.

Kiiza amesema mwaka huu wanatarajia kushiriki wageni kutoka zaidi ya mataifa tisa, yakiwemo Ujerumani, Italia, Ghana, Rwanda, Kenya, Uganda na Uingereza.

BAG 02

Ameeleza kuwa, maonesho yanayofanyika ni pamoja na muziki, maigizo, ngoma za kiasili na maonesho ya bendi, huku wataalamu kutoka Uingereza wakitarajiwa kutoa msaada wa kiufundi katika maeneo ya ubunifu na utangazaji.

Kwa mujibu wa Kiiza, moja ya faida kubwa za tamasha hilo ni kuitangaza Taasisi ya Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) na shughuli zake kwa umma.

Katika siku ya kwanza, Oktoba 28, 2026, shughuli za tamasha zilipangwa kuanza kwa ufunguzi rasmi katika jukwaa kuu la nje kuanzia saa 1:00 usiku.

BAG 03

Miongoni mwa vikundi vilivyokuwa kwenye ratiba ni Anga Zetu kutoka Dar es Salaam, Sauti ya Umoja na Bagamoyo Collective, kabla ya shughuli za ufunguzi rasmi zilizohusisha Buyegu Theatre Group, Mundu Arts Group na Gen Z Mnanda.

Burudani nyingine zilihusisha Bwagamoyo Africulture, Makirikiri wa Tanzania, Freedom Band, Elie Ongala Nyembo na Jeremie Tshibi kutoka Congo, huku Nasybite akitarajiwa kuhitimisha ratiba ya usiku kwa muziki wa Singeli.

Katika siku ya pili Oktoba 29, 2026, ratiba iliendelea kutoa nafasi kwa maonesho ya aina mbalimbali, yakiwemo ya Mzee wa sanaa za asili Matwi Ga Chalo kutoka Ukerewe, Eli Kanogoleke na TaSUBa Band, Mzinga Band pamoja na vikundi vya sarakasi na maigizo.

BAG 04

Mbali na maonesho hayo, jukwaa la Mwembeni lilikuwa na nafasi maalumu ya kuonesha filamu chini ya Bodi ya Filamu.

Ratiba ya Ijumaa Oktoba 30, 2026 imeendelea kuonesha mchanganyiko wa vipaji, ikihusisha Talent Search and Empowerment, Tanzania Education Theatre, Jilema Shija, Zillas Art Production kutoka Kenya na Russian Cultural Center kwa kushirikiana na AFASR.

Kwa upande wa burudani za usiku, waliopangwa ni Mtifi wa Afrika, Napsa Theater kutoka Zambia, Nahabwe Keneth kutoka Uganda, Poa Arts Group kutoka Zanzibar, Afro Mob African Dance, Regina Beraldo Kihwele maarufu Gynah na Mtoto wa Mungu.

BAG 05

Siku ya mwisho ya tamasha, Jumamosi Oktoba 31, shughuli zinatarajiwa kuanza mapema katika jukwaa la ndani kuanzia saa 8:00 mchana.

Wasanii na vikundi vilivyopangwa ni Best Culture Quality Music kutoka Mkuranga, Mahanze kutoka Dodoma, TaSUBa Students, Kigamboni Community Charity (KCC), Tabasamu Music Band na China Tanzania Cultural Centre kwa kushirikiana na AFASR.

Wakati huohuo, kuanzia saa 12:30 jioni hadi saa 2:00 usiku, kutakuwa na maonesho ya filamu katika jukwaa la Mwembeni.

BAG 06

Kilele cha tamasha kinatarajiwa kufanyika katika jukwaa kuu la nje kuanzia saa 1:00 usiku, ikitanguliwa na maonesho ya Landaa Cultural Group, Kikundi cha Utamaduni cha Kusini, Sauti ya Umoja na Kandiri Art Group.

Shughuli za kufunga tamasha rasmi zinatarajiwa kuhusisha Bagamoyo Acrobatic Club, Magomamoto Theatre Group na Sauti ya Umoja, pamoja na mgeni rasmi.

Baada ya hapo burudani itaendelea kupitia Magomamoto Theatre Group, Safi Theater Group, Gifted Muneka kutoka Zambia, Mose Iyobo na Iyobo’s Family, Ras Gwandumi na Bongo Roots, Sauti Marley na The Band, Baob Cypher, Siza Segere Stars, Vitali Maembe na Watupamawe.

Ratiba hiyo inatarajiwa kufungwa na Ziro MC 77 atakayepanda jukwaani kwa burudani ya Singeli saa 10:25 alfajiri ya Novemba Mosi, 2026.