Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baada ya ukimya wa 40 ya mtoto wake, Wema Sepetu afunguka

WEMA Pict


Baada ya siku kadhaa kuibuka maswali kuhusu kutofanyika kwa sherehe ya siku 40 ya mtoto wake wa kiume, staa wa filamu Tanzania, Wema Sepetu, hatimaye amevunja ukimya na kuweka wazi kilichokuwa kinaendelea nyuma ya pazia.


Kupitia Instagram Story yake aliyoiweka leo, Wema amewashukia watu waliokuwa wakiendelea kuhoji kuhusu sherehe hiyo, akidai wamekuwa wakitafuta kosa dhidi yake tangu alipofanya Aqiyqah ya mwanae.


"Haya nyie waja mnaodai 40 mtasema mtoto wa kwenu... Mbona kama mapovu yanawatoka sana... Mmenikosa kosa kwenye Aqiyqah ndo mlitaka kuja kunimaliza sio... Mnikome...!!!"

Baada ya ujumbe huo, aliandika tena: "Sasa mkae kwa kutulia... EBO...!!!"

Hata hivyo, Wema hakusimamia hapo. Katika ujumbe mwingine, alifichua kuwa kwa siku kadhaa amekuwa akisumbuliwa na matatizo makubwa ya afya yaliyomfanya ahofie hata maisha yake.

"Nimeumwa magonjwa ya ajabu ajabu... Nikajua nakufa..."

Akiambatanisha picha akiwa amelazwa hospitalini akiwekewa dripu, Wema ameandika: "Nimelazwa baada ya Aqiqah tu ya mtoto since last Monday..."

Kauli hizo zimekuja siku chache baada ya kuzuka kwa mjadala kuhusu ukimya wa sherehe ya siku 40 ya mtoto wake, ambayo awali ilikuwa imepangwa kufanyika Julai 23, 2026 katika ukumbi wa SuperDome, Masaki, jijini Dar es Salaam. 

Kabla ya tarehe hiyo, Wema alikuwa ametangaza viingilio vya hafla hiyo, hatua iliyozua mjadala mkubwa mitandaoni.

Hata hivyo, Julai 23 ilipofika, sherehe hiyo haikufanyika kama ilivyokuwa imepangwa na hakukuwa na maelezo rasmi kutoka kwa Wema au watu wake wa karibu, jambo lililozua maswali mengi kutoka kwa mashabiki na wadau wa burudani.

Wema alijifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume Juni 12, 2026, tukio lililopokelewa kwa furaha kubwa baada ya safari ndefu ya kusubiri kutimiza ndoto yake ya kuwa mama. 

Kabla ya siku ya 40, familia hiyo ilifanya Aqiyqah ya mtoto wao Julai 16, lakini sasa Wema amesema mara baada ya ibada hiyo alianza kuugua na hali yake ikawa mbaya kiasi cha kulazwa hospitalini kwa matibabu. 

Kupitia maelezo yake ya leo, Wema ameashiria kuwa changamoto za afya ndizo zilizosababisha mipango yake kubadilika, huku akiwataka wanaoendelea kuzungumzia siku 40 ya mwanae kuacha kufanya hivyo.

Baada ya ujumbe huo kusambaa, mashabiki na watu mbalimbali wameendelea kumtakia apone haraka, huku wengi wakieleza kufarijika baada ya kufahamu sababu ya ukimya uliogubika sherehe iliyokuwa ikisubiriwa na wengi.