Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wema Sepetu afafanua Sh5 Milioni za kumuona Ollie

WEMA Pict

Muktasari:

  • Wema ametangaza kuwa, sherehe hiyo ya kumshukuru Mungu kwa hatua ya siku 40 ya mtoto wake itafanyika Julai 23, 2026 katika ukumbi wa The SuperDome, Masaki jijini Dar es Salaam.

BAADA ya kutangaza viingilio vya sherehe ya arobaini ya mtoto wake, Ollie, muigizaji na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, amefafanua kuhusu bei hizo ambazo zimezua mjadala kwa baadhi ya mashabiki wake mitandaoni.

Wema ametangaza kuwa, sherehe hiyo ya kumshukuru Mungu kwa hatua ya siku 40 ya mtoto wake itafanyika Julai 23, 2026 katika ukumbi wa The SuperDome, Masaki jijini Dar es Salaam.

Tangazo la viingilio hivyo limeibua maoni mbalimbali, hasa baada ya kufahamika kuwa kifurushi cha juu zaidi cha kushiriki tukio hilo kinafikia Sh5 milioni, huku baadhi ya mashabiki wakiona kiwango hicho ni kikubwa kwa tukio ambalo linahusisha mtoto wa msanii mwenye mashabiki wengi.

WEM 01
WEM 01

Akizungumza na Mwanaspoti, Wema Sepetu amesema hakuna tatizo katika viwango hivyo kwa sababu vimewekwa kwa namna ambayo kila mtu ataweza kushiriki kulingana na uwezo wake.

Wema amefafanua kuwa ndiyo maana wameweka bei tofauti, ili kila anayetamani kuwa sehemu ya tukio hilo aweze kuchagua kiwango kinachomfaa.

“Acha iwe hivyo jamani, mbona hakuna shida. Kuna bei tofauti tofauti, kila mtu ataingia sehemu ambayo uwezo wake unamruhusu, nawapenda mashabiki zangu na natamani siku hiyo wajitokeze kwa wingi kufurahia kwa pamoja, wasilalamike sana jamani, waje tu,” amesema Wema.

Sherehe hiyo inakuja baada ya Wema na mchumba wake, mwanamuziki Whozu, kupata mtoto wao wa kwanza, Ollie, ambaye amekuwa gumzo tangu kuzaliwa kwake kutokana na umaarufu wa wazazi wake katika tasnia ya burudani.

WEM 02

Juni 23, 2026, Wema alijifungua mtoto huyo, tukio ambalo lilipokewa kwa furaha kubwa na mashabiki wake baada ya safari ndefu ya kusubiri kupata mtoto.

Kabla ya sherehe ya arobaini, Julai 16, 2026 familia hiyo ilifanya pia hafla ya hakika ya Ollie, iliyofanyika nyumbani kwa mama wa Wema Sepetu eneo la Sinza jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kumshukuru Mungu mtoto kuzaliwa.

Kwa mujibu wa tangazo la Wema, viingilio vya sherehe ya Julai 23 vimepangwa katika viwango mbalimbali ambavyo ni Sh100,000, Sh300,000, Sh500,000, huku kiwango cha juu zaidi kikiwa Sh5 milioni kwa wageni watakaopendelea huduma maalumu.

Tangu kutangazwa kwa viingilio hivyo, mashabiki wameendelea kutoa maoni tofauti, huku wengine wakisema ni gharama kubwa na wengine wakisisitiza kuwa ni uamuzi wa familia kuweka viwango hivyo kwa tukio lao.

Hata hivyo, Wema anaonekana kusimama na mpangilio huo akisisitiza kuwa lengo ni kumpa kila mtu nafasi ya kushiriki kwa kiwango anachoweza, huku maandalizi ya sherehe hiyo yakitarajiwa kuwa miongoni mwa matukio makubwa ya burudani na mastaa jijini Dar es Salaam.