Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AY na Banza watoa ujumbe mzito

AY

MWANDISHI WETU WANAMUZIKI maarufu nchini AY na Banzastone wamewaonya mashabiki kutofuata mkumbo katika kufanya maamuzi kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba. Kampeni za uchaguzi mkuu zimeanza rasmi ambapo kila kukicha kumekuwa kukiibuka mambo mapya huku kila mgombea wa nafasi iwe urais, ubunge au udiwani akiingia na staili mpya. Lakini AY, ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya aliiambia Mwanaspoti kuwa huu ni wakati muafaka kwa vijana nchini kutumia nafasi zao za kupiga kura kufanya mabadiliko ya kweli. "Watu wasifuate mkumbo kila mtu atumie vizuri nafasi yake kufanya maamuzi ambayo anayaona ni sahihi, mtu asikubali kushawishiwa na mtu mwingine. "Wajitokeze pia kwa wingi kusikiliza kampeni na siku ya uchaguzi waende kufanya maamuzi sahihi, tunahitaji mabadiliko na watu sahihi wenye uwezo wa kuongoza hii nchi kutuletea maendeleo," alisema msanii huyo, ambaye amejijengea jina kwenye nchi za Afrika Mashariki na Kati katika miaka ya hivi karibuni. Banza, nguli katika dansi la Tanzania alisema huu ndio muda muafaka kwa wapiga kura na kufanya mabadiliko kwa manufaa ya Tanzania na watu wanapaswa kuwa makini. "Uchaguzi ndio kitu muhimu kila aliyejiandikisha atumie haki yake ya msingi kuna mambo mengi, ambayo yamekuwa yakilalamikiwa, huu ndiyo wakati muafaka wa kuyabadilisha kwa kupiga kura kuchagua watu makini."