Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aslay afichua kinachombeba

ASLAY Pict

Muktasari:

  • Pamoja na kuwa msanii huyo ameendelea kutoa kazi mpya na anaamini baadhi yake ni bora zaidi, mashabiki wake bado humrudisha kwenye enzi zilizompa jina kubwa zaidi.

KAMA kuna jambo Aslay hawezi kulikwepa akipanda jukwaani kwa sasa, basi ni nyimbo zake za zamani.



Pamoja na kuwa msanii huyo ameendelea kutoa kazi mpya na anaamini baadhi yake ni bora zaidi, mashabiki wake bado humrudisha kwenye enzi zilizompa jina kubwa zaidi.

Aslay aliIiambia Mwanaspoti mashabiki hawaridhiki anapofanya shoo bila kuwapigia baadhi ya nyimbo zake za zamani, jambo analosema linampa picha ya nguvu ambazo kazi hizo bado zina kwenye mioyo yao.

“Nyimbo zile ndizo zinazonibeba, kuna nyimbo nyingi nimezitoa na bado naendelea kutoa ambazo ni nzuri zaidi, ila mashabiki ukipanda jukwaani bila kuwaambia nyimbo zile za zamani hawaridhiki. Wanasumbua kuomba zipigwe na ukiimba, vibe unaiona hasa kwa mashabiki,” amesemsa Aslay.

ASLA 01

Nyimbo kama Mhudumu, Pusha, Natamba na Likizo ni miongoni mwa kazi zilizokuwa sehemu muhimu ya safari yake ya mwanzo ya muziki wa solo baada ya kutoka Yamoto Band.

Aslay amesemsa hata anapopanda kwenye majukwaa madogo au kufanya shoo za maeneo ambayo si makubwa kama zamani, mashabiki bado humtaka awapeleke kwenye nyimbo hizo.

Akizungumzia shoo anazofanya, Aslay amesemsa jambo kubwa kwake si ukubwa wa eneo analopanda, bali mwitikio anaoupata kutoka kwa mashabiki.

Alieleza kuwa hata akiwa kwenye shoo ndogo, mashabiki bado humsukuma kuimba nyimbo zake za zamani na mara nyingi ndipo anapoona nguvu yake halisi.

ASLA 02

“Ukiimba, vibe unaiona hasa kwa mashabiki,” amesemsa Aslay, akieleza namna anavyoweza kutambua nyimbo ambazo bado zina nguvu pale anapokuwa mbele ya mashabiki.

Hata hivyo, mashabiki wake wanaonekana kuwa na msimamo wao. Wanataka kusikia Aslay wa sasa, pia hawataki wa zamani apotee.

ASLA 03

Ndiyo maana kila anapopanda jukwaani, nyimbo hizo za zamani huibuka tena kupitia maombi ya mashabiki.

Na kwa Aslay, hilo ndilo jibu linalomfanya aamini kazi alizowahi kufanya miaka iliyopita bado zina nafasi kubwa. Kwa kifupi, muziki mpya unaweza kuwa safari yake ya sasa, lakini nyimbo za zamani bado ndizo zinazompa nguvu kubwa jukwaani.