Manula: Kuwafunga DR Congo imetupa hatua nyingine

Muktasari:
- Manula anasema DR Congo,wapo nafasi nzuri kwenye kiwango cha ubora Afrika,hivyo kuifunga imewatangazia sifa nzuri katika mataifa mengine.
KIPA wa Taifa Stars, Aishi Manula amesema kitendo cha kuifunga DR Congo katika mechi ya kirafiki ya kimataifa,kimewafanya wajiamini na kuona wanaweza kupambana.
Manula anasema DR Congo,wapo nafasi nzuri kwenye kiwango cha ubora Afrika,hivyo kuifunga imewatangazia sifa nzuri katika mataifa mengine.
"DR Congo,wapo nafasi nzuri kwenye viwango vya ubora Afrika,imetupa ujasiri kuona tuendelee kupambana ipo siku tutakuja kufika mbali kama ilivyo kwa wengine ambao wanashiriki Kombe la Dunia,"anasema.
Manula anasema wamejifunza ufundi namna ambavyo DR Congo,wameonyesha kupambana mpaka dakika ya mwisho,licha ya kufungwa