Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alliance FC yaja na nyota kutoka DR Congo, Rwanda

Muktasari:

Alliance itaanza kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu Bara dhidi ya majirani zao wa Mbao Fc kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kabla ya kuivaa African Lyon kwenye Uwanja wa Nyamagana.

Mwanza. Alliance FC imesajili wachezaji wapya 29, wakiwemo na nyota wawili wa kigeni kutoka DR Congo na Rwanda tayari kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu Bara Agosti 22, 2018.

Wachezaji hao wa kulipwa wawili ni Chinedu Michael kutoka DR Congo na Weyaka Tatue (Rwanda), watakuwa na kibarua cha kuhakikisha timu hiyo inakuwa tishio msimu ujao wa Ligi Kuu.

Alliance FC ni zao wa shule ya kukuzia vipaji ya jijini Mwanza imepanda daraja msimu huu mwa mara ya kwanza huku nyota wake wengi wakiwa kutoka katika Akademi yao.

 Alliance itaanza kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu Bara dhidi ya majirani zao wa Mbao Fc kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kabla ya kuivaa African Lyon kwenye Uwanja wa Nyamagana.

Alliance itacheza mechi yake ya kwanza ugenini mkoani Mbeya dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine.

Wachezaji waliosajiliwa na Alliance msimu huu: Said Rubava, Ibrahim Isihaka, Kelvin Richard, Godfrey Ndumule, Israel Patrick, Hans Masoud, Kelvin Kindwanga, Joseph James, Wema Sadock, Godfrey Luseke na Nteze John.

Wengine ni Shaban William, Juma Nyange, Ismail Zumma, Samir Vicent, Richard John, Martin Kiggy, Maganda Nchembe, David Richard, Siraji Juma, Jamari Soud, Mapinduzi Balama, Zabona Khamis, Rashid Ruava, Rajabu Ramadhan, Juhudi Philimon, Chinedu Michael na Weyaka Tatue