Snura apata dawa mastaa wanaopenda kiki

Muktasari:
Snura amesema, pasipo kuwataja majina, anashangazwa na tabia ya mastaa wengi kuwa ‘bize’ kutafuta kiki kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii badala ya kukutana pamoja na kufikiria ni kitu gani wanaweza kufanya ili waendelee kimaisha.
STAA wa muziki na mtaalamu wa kukata nyonga, Snura amefunguka kuwa mastaa wengi wanapenda kiki kuliko kusaka fedha kitu ambacho yeye hakifanyi hicho.
Snura amesema, pasipo kuwataja majina, anashangazwa na tabia ya mastaa wengi kuwa ‘bize’ kutafuta kiki kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii badala ya kukutana pamoja na kufikiria ni kitu gani wanaweza kufanya ili waendelee kimaisha.
“Jamani mimi nashangaa siku hizi huku mjini mastaa wanatafuta kiki sana kuliko kufikiria mbinu ya kusaka hela yaani ni shida kabisa, tubadilike jamani, muda unakwenda,” alisema Snura.
Hata hivyo, Snura amesema anajivunia kupata kiki kutokana na ubunifu wa staili yake ya uchezaji na kujituma akiwa stejini na ndio maana hana skendo za ajabu.