Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zigo la Manji latua kwa Tenga

Muktasari:

  • YANGA imeamua kuutua mzigo wa mzozo wao na TFF juu ya Uchaguzi wa kuziba nafasi zilizowazi kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, lakini huku Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezom, Dk Harrison Mwakyembe akiutupa mpira kwa Mwenyekiti wa BMT, Leodegar Tenga.

WAKATI zoezi la kuchukua na kurudisha fomu likifungwa rasmi jana saa 10:00 jioni sakata la uchaguzi huo bado linaonekana kuwa, gumu kwani hesabu zinaonyesha linahamia mikononi mwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo, Leodegar Tenga.

Lakini mambo yakiwa hivyo, tayari ishu nzima ya mzozo huo wa Yanga wa kumtaka Manji dhidi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumgomea limetua mikononi mwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alidaiwa kuahidi kuingilia kati.

Yanga waliamua kuufikisha mzozo wao na TFF juu ya uchaguzi wao wa kuziba nafasi zilizo wazi, walipoalikwa na Waziri Mkuu kwenda kucheza na Namungo FC na mechi kwisha kwa sare ya 1-1.

Hebu tuanze na ishu ya pale BMT. Taaarifa iliyotolewa jana Jumatatu inasema baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kuona mambo si mambo alisema endapo utata huo utahamia kwa Mwenyekiti wa BMT, Leodegar Tenga anaamini haitakuwa njia mbaya.

Mwakyembe alisema bado suala hilo sio gumu kwa sasa na kwamba kama kweli Yanga wamejipanga kulipeleka kwa Tenga bosi huyo wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) anaweza kufanya kitu kumnaliza utata huo.

Alisema anachotaka yeye ni kuona ofisi yake inakuwa ya mwisho kuamua kesi hiyo na kwamba mvutano huo unawasumbua Wanayanga ni juu ya uchaguzi kutosimamiwa na Kamati yao ya uchaguzi iliyo chini ya Sam Mapambe na pia juu ya nafasi ya mwenyekiti wao wanaomtaka Yusuf Manji.

“Nimesikia upande mmoja unataka kwenda BMT nimefurahi sana waende wakae chini ya mwanasoka mzoefu Tenga (Leodegar) awasikilize pande zote mbili kuna shida gani ikishindikana pale litakuja kwangu,” alisema Dk Mwakyembe.

“Mimi naamini hili ni suala la kutumia busara tu, sioni kama ni gumu halina ugumu wowote wanachoshindana ni mambo mawili kwanza wanataka kamati yao ya uchaguzi ndio isimamie uchaguzi na TFF wanasema mbona hamtoshi, ni mvutano huo sasa tutaangalia kama wanaweza au kama hawawezi tutafanya maamuzi.

“Pili ni kuhusu Yusuf Manji hakuna anayekataa kwamba Wanayanga wanampenda sana, lakini katika nchi kuna kanuni na sheria hata kama unampenda, we mpende nyumbani kwako unapokuwa kwenye nchi kuna sheria, lazima tuangalie kuna kitu gani Yanga wanataka na sheria pia.

SAKATA LATUA KWA MAJALIWA

Kule Ruangwa, mkoani Lindi juzi Jumapili mara baada ya mchezo wa Namungo dhidi ya Yanga, mabosi wa Jangwani walikutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kumuelezea kinagaubaga juu ya mzozo wao na Shirikisho la Soka (TFF).

Ingawa viongozi wa Yanga wamekuwa wazito kuzungumzia yaliyojiri huku kwa Waziri Mkuu, lakini taarifa za ndani zinasema kuwa, sakata hilo la Manji na uchaguzi wa Yanga liliwasilishwa mezani kwa kigogo huyo na kuwaahidi kulifanyia kazi.

Hata hivyo bado haijajulikana kipi kilihitimishwa na Waziri Mkuu huyo ambaye ni mmoja ya wanamichezo maarufu akiwa na taaluma ya Ukocha, lakini mmoja wa vigogo wa klabu hiyo alisema; ‘Subirini mtajulishwa na mamlaka husika juu ya kilichojadiliwa na maamuzi yaliyotolewa.”

ZITTO AIUMA SIKIO

Katika hatua nyingine, Mwanasiasa mchachari nchini na mwanachama wa Simba, Zitto Kabwe amewapa akili watani zao, Yanga kama wanataka kwenda na wakati katika kasi ya soka la dunia ya kileo.

Zitto alisema ili Yanga iwe kisasa sio lazima iwaige Simba, lakini inaweza kubadilisha mfumo wa uendeshaji wake iendelee kutisha nchini.

Mbunge huyo wa Kigoma Mjini, alitoa kauli hiyo alipoulizwa anadhani Yanga ifanye nini ili iondokane na hali iliyonayo sasa.

“Klabu ya Yanga ni klabu kubwa na inaweza kuleta ushindani kwenye soka iwapo itaongozwa vizuri.

“Ningependa Yanga iendelee kuwa klabu ya Wananchi, lakini iendeshwe kisasa.

“Sio lazima wawe kama Simba ya sasa Lakini wanaweza kuendeshwa na menejimenti ya kukodisha (management contract).”