Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga burudani imerudi

YANGA Pict

Muktasari:

  • Yanga imelazimika kutoka nyuma kuja kutengeneza ushindi huo baada ya kushtuliwa mapema ikiruhusu bao dakika ya saba kwa  la mshambuliaji wao wa zamani, Crispin Ngushi akipokea pasi safi ya Harun Chanongo.

YANGA imerudi katika njia ya ushindi baada ya kuichapa Mashujaa mabao 2-1, lakini mashabiki wakaibua hoja, soka la burudani limerejea.

Yanga imelazimika kutoka nyuma kuja kutengeneza ushindi huo baada ya kushtuliwa mapema ikiruhusu bao dakika ya saba kwa  la mshambuliaji wao wa zamani, Crispin Ngushi akipokea pasi safi ya Harun Chanongo.

Bao hilo likawaongezea nguvu Yanga na kuzidisha mashambulizi ikiwachezesha nusu eneo Mashujaa kwa mashambulizi makali.

Dakika ya 16, Peter Shalulile alikaribia kuisawazishia timu yake lakini akashindwa kutumia pasi safi aliyotengenezewa na beki wake, Ibrahim  Kazimoto.

YANG 01

Dakika ya 22, Yanga ikasawazisha bao hilo,Shalulile akirekebisha makosa yake akifunga bao kwa shuti kali akipokea asisti ya Stephanie Aziz KI.

Hilo linakuwa bao la pili kwa wawili hao na ni kama walirudia walichofanya kwenye mechi dhidi ya Fountain Gate na Azizi KI alimtengenezea pasi safi iliyotumiwa na mshambuliaji huyo wa zamani wa Mamelodi Sundowns.

Kocha wa muda wa Yanga, Sydney Dladla alionyesha mabadiliko kwa kikosi chake na  kilionekana kutawala mchezo huo kwa pasi nyingi huku ikionekena kutengeneza hesabu za mashambulizi makali na  hadi mapumziko timu hizo zikifungana bao 1-1.

Yanga ilirudi na nguvu ileile kipindi cha pili ikiendelea kuishambulia Mashujaa ambayo ni kama iliamua kukaa nyuma ikisubiri kutengeneza mashambulizi ya kushtukiza.

Dakika ya 70, Yanga ikafanya mabadiliko mawili ikiwatoa Juma Issa na Farouk Koumara nafasi zao zilichukuliwa na Aziz Andambwile na Clement Mzize.

YANG 02

Mabadiliko hayo yakaingiza bao la pili kwa Yanga, Mzize akifunga bao zuri akimchambua kipa Mussa Malika akitumia asisti ya Housseine Zakouani.

Hilo linakuwa bao la kwanza kwa Mzize  tngu arejee uwanjani  baada ya kuwa nje kwa muda akiuguza majeraha aliyopata msimu uliopita, akifungua akaunti yake ya mabao.

Yanga ikaendelea kuishambulia Mashujaa kwa nguvu, lakini utulivu wa kutumia nafasi hizo ukawa mdogo na hadi mwisho wa mechi wenyeji wakaibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuendelea kuwa mbabe wa Mashujaa ikishinda mechi zote saba ilizowahi kukutana  dhidi ya wanajeshi hao, ikifunga jumla ya mabao 21, huku Mashujaa ikifunga manne. 

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi  22 ikisalia nafasi ya pili, baada ya kucheza mechi tisa huku vinara wakiendelea kuwa Simba wenye pointi 24.