Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Namungo aibukia Simba, akipewa Ukurugenzi wa Ufundi

Picha na Simba

Muktasari:

  • Amewahi kuifundisha timu ya Taifa ya Zambia kuanzia Agosti 2014 hadi Machi 2015 na aliwahi kuiongoza katika Fainali za AFCON mara moja.

Simba leo Jumanne, Oktoba, 27, 2026 imemtangaza rasmi Honor Janza kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Klabu hiyo.

Nafasi hiyo ni mpya na kwa mara ya kwanza imeanza kuwepo ndani ya klabu ya Simba.

Janza ana uzoefu mkubwa na soka la Tanzania kwani amewahi kuwa Kocha Mkuu wa Namungo FC aliyojiunga nayo Desemba 2021.

Akiwa Namungo FC, aliwahi kushinda mara moja Tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Agosti 2022, Janza aliteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa muda wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Amewahi kuifundisha timu ya Taifa ya Zambia kuanzia Agosti 2014 hadi Machi 2015 na aliwahi kuiongoza katika Fainali za AFCON mara moja.

Kocha huyo ana leseni ya daraja la juu ya Ukoch ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Pia ni miongoni mwa wakufunzi wa makocha wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) na siku chache kabla ya kujiunga Simba alikuwa katika kituo cha Ufundi cha TFF, Mnyanjani Tanga, akiwafundisha makocha wa ngazi tofauti za leseni Tanzania.