Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waarabu wafanya kufuru kwa Lewandowski

LEWANDO Pict

Muktasari:

  • Ingawa katika wiki za karibuni Lewandowski amehusishwa na klabu mbalimbali ikiwemo Juventus, AC Milan pamoja na klabu ya Marekani ya Chicago Fire FC, Al-Hilal ndiyo inaonekana kuwa mbele zaidi katika mbio hizo.

BARCELONA, HISPANIA: MSHAMBULIAJI mkongwe wa Barcelona, Robert Lewandowski, anakaribia kuachana na klabu hiyo katika dirisha lijalo na kujiunga na Al-Hilal kutoka Ligi Kuu ya Saudi Arabia.

Straika huyo anaripotiwa kuwa karibu kukubali ofa kubwa ya klabu hiyo ya Saudia inayotamani sana kuipata saini yake.

Kwa mujibu wa WP Sportowe Fakty, klabu hiyo yenye makao yake makuu Jijini Riyadh limedhamiria kuipata saini yake ili kuongeza nguvu katika safu yao ya ushambuliaji kuelekea msimu ujao.

Ingawa katika wiki za karibuni Lewandowski amehusishwa na klabu mbalimbali ikiwemo Juventus, AC Milan pamoja na klabu ya Marekani ya Chicago Fire FC, Al-Hilal ndiyo inaonekana kuwa mbele zaidi katika mbio hizo.

LEWA 01

Lewandowski anaripotiwa kupewa ofa ya mshahara wa Euro 90 milioni ( zaidi ya shilingi 274 bilioni) kwa msimu ili akubali kuhamia Saudi Arabia kujiunga na matajiri hao.

Licha ya ripoti za awali kutoka gazeti la Hispania la AS kudai kuwa sababu za kisiasa na kiusalama huenda zingemzuia nyota huyo kwenda Mashariki ya Kati, ukubwa wa ofa hiyo unaonekana kubadili kabisa mwelekeo wa mambo.

LEWA 02

Aidha, kutokana na changamoto za kifedha zinazoikabili Barcelona, kuondoka kwa mchezaji wao anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kunaweza kupunguza mzigo mkubwa wa matumizi ya timu.

Iwapo Lewandowski atajiunga na Al-Hilal, atakuwa sehemu ya kikosi chenye nyota wengi kinachonolewa na kocha wa zamani wa Inter Milan, Simone Inzaghi kwani hadi sasa timu hiyo ina nyota kadhaa akiwemo mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid na mshindi wa Ballon d'Or, Karim Benzema, pamoja na Sergej Milinkovic-Savic, Theo Hernandez, Darwin Nunez, Ruben Neves na Kalidou Koulibaly ambao kabla walitamba kwenye soka la Ulaya.