Vozihna aanza maisha mapya Chile, kanuni ya Ligi ikivunjwa
Muktasari:
- Vozihna anajiunga na Colo-Colo, ambayo ndiyo klabu yenye mafanikio makubwa zaidi nchini Chile, akiwa mchezaji huru baada ya kutumia misimu miwili iliyopita katika klabu ya Chaves inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Ureno, ambako alikuwa akiingia na kutoka kwenye kikosi mara kwa mara.
Kipa wa Cape Verde aliyejizolea umaarufu kwenye mashindano ya Kombe la Dunia 2026, Josimar José Évora Dias maarufu kwa jina la Vozihna (40), ameanza maisha mapya Chile baada ya kujiunga na klabu ya Colo-Colo inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.
Vozihna anajiunga na Colo-Colo, ambayo ndiyo klabu yenye mafanikio makubwa zaidi nchini Chile, akiwa mchezaji huru baada ya kutumia misimu miwili iliyopita katika klabu ya Chaves inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Ureno, ambako alikuwa akiingia na kutoka kwenye kikosi mara kwa mara.
Kipa huyo alipata umaarufu mkubwa duniani, baada ya kuiwezesha Cape Verde kutoruhusu bao dhidi ya mabingwa wa Kombe la Dunia, Hispania, katika mchezo wa hatua ya makundi kwenye mashindano hayo, akifanya mfululizo wa sevu za kiwango cha juu katika kipigo cha maumivu cha mabao 3-2 dhidi ya Argentina baada ya muda wa nyongeza.
Akiwa Colo-Colo, Vozinha ataruhusiwa kutumia jina lake la utani mgongoni mwa jezi yake baada ya Shirikisho la Soka la Chile (ANFP) kupitisha kwa kauli moja uamuzi wa kufanya msamaha maalumu dhidi ya kanuni za sasa.
Kwa mujibu wa kanuni za ligi hiyo, wachezaji wanapaswa kuvaa majina yao ya ukoo pekee mgongoni mwa jezi. Hata hivyo, viongozi wakuu wa klabu mbalimbali nchini Chile waliunga mkono ombi hilo kwa niaba ya Vozinha, ambaye jina lake kamili ni Josimar José Évora Dias.