Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo Man United bado wanajikongoja kwa Delap

Muktasari:

  • Delap ambaye msimu huu amecheza mechi 26 za michuano yote na kufunga mabao 10, anauzwa kwa kiasi kisichopungua Pauni 40 milioni.

MANCHESTER United inapambana kuhakikisha inaipata saini ya mshambuliaji wa Ipswich Town na England, Liam Delap katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi licha ya kumuweka katika rada zao Victor Osimhen.

Delap ambaye msimu huu amecheza mechi 26 za michuano yote na kufunga mabao 10, anauzwa kwa kiasi kisichopungua Pauni 40 milioni.

Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo unatarajiwa kumalizika 2029 na Ipswich inadaiwa kutaka kumsainisha mkataba mpya ili kumuuza kwa pesa nyingi zaidi ifikapo dirisha lijalo.

Ili kuipata huduma yake, Man United inatakiwa kushinda vita pia dhidi ya timu nyingine za ndani na nje ya England ikiwemo Chelsea.


Alexander Isak

LIVERPOOL inataka kumtoa mshambuliaji wake raia wa  Uruguay, Darwin Nunez, 25, kama sehemu ya ofa ya kuipata saini ya mshambuliaji wa Newcastle United na timu ya taifa ya Sweden, Alexander Isak, 25, ambaye msimu huu amecheza mechi 17 za Ligi Kuu England. Mbali ya kumtoa Nunez kama ofa, Liverpool pia inataka kuweka kiasi cha pesa ili kuishawishi Newcastle kumwachia mchezaji huyo.


Hugo Ekitike

ARSENAL na Chelsea zipo kwenye vita kali ya kutaka kumsajili straika wa Eintracht Frankfurt na Ufaransa, Hugo Ekitike, 22, dirisha lijalo la majira ya kiangazi mara tu litakapofunguliwa huko Ulaya. Ekitike ambaye msimu huu amecheza mechi 32 za michuano yote na kufunga mabao 17, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika ifikapo 2029.


Frenkie de Jong

INAELEZWA Liverpool inataka kufanya kazi ya ziada katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kuboresha kikosi na moja kati ya majina ambayo benchi la ufundi limeyaweka katika mpango kazi ni la kiungo wa Barcelona na Uholanzi, Frenkie de Jong, 27, ambaye hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha timu yake. Mkataba wa De Jong unatarajiwa kumalizika 2027.


Maximo Perrone

KIUNGO wa Manchester City na Argentina, Maximo Perrone, 22, anayecheza kwa mkopo Como ya Italia anatarajiwa kusaini mkataba wa kudumu wa kuendelea kuitumikia timu hiyo na tayari ameshaanza mazungumzo na vigogo ambao wamevutiwa na kiwango alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu. Mkataba wake wa sasa na Man City unatarajiwa kumalizika 2028.


Kaoru Mitoma

BRIGHTON haina mapango wa kumuuza mshambuliaji raia wa Japan, Kaoru Mitoma, 27, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi licha ya kuwa mkataba wake umebakisha miaka miwili. Katika dirisha lililopita la majira ya baridi alihusishwa na Al Nassr ya Saudi Arabia iliyokuwa tayari kutoa Pauni 80 milioni. Msimu huu Mitoma amecheza mechi 28.


Tijjani Reijnders

KIUNGO wa AC Milan  na Uholanzi, Tijjani Reijnders, 26, anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika viunga hivyo kwenye mkataba ambao unatarajiwa kumalizika 2030. Reijnders ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2028, ni mmoja kati ya viungo tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Milan.


Fermin Lopez

ASTON Villa bado inataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Hispania, Fermin Lopez, 21, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kushindwa kufanya hivyo katika dirisha lililopita la majira ya baridi. Awali katika dirisha lililopita, Villa ilikuwa tayari kulipa  Euro 70 milioni kwa ajili ya kuipata huduma yake. Lopez ni mmoja kati ya mastaa ambao wameonyesha kiwango bora tangu kuanza msimu huu.