Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo Barca waanza kazi kwa Luis Diaz

TETESI Pict

Muktasari:

  • Diaz ambaye msimu uliomalizika alicheza mechi 50 za michuano yote na kufunga mabao 17, mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2027.

BARCELONA imeanza mazungumzo ya awali ya kumsajili winga wa Liverpool, Luis Diaz, 28, katika dirisha hili la usajili huko Ukaya, lakini inakumbana na upinzani mkubwa kutoka katika timu za Saudi Arabia ambazo pia zinahitaji huduma yake.

Diaz ambaye msimu uliomalizika alicheza mechi 50 za michuano yote na kufunga mabao 17, mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2027.

Hata hivyo, wikiendi iliyopita mchumba wa staa huyo, Gera Ponce aliandika ujumbe katika kurasa zake za mitandao ya kijamii uliokuwa ukiwashukuru mashabiki wa Liverpool kwa ukarimu wao katika kipindi chote ambacho yeye na Diaz wamekuwepo jijini Liverpool.

Ujumbe huo ambao ulitafsiriwa kama sehemu ya mkono wa kwaheri, mashabiki wengi wanaamini msimu uliomalizika ndio ulikuwa wa mwisho kwa Diaz ambaye ndoto yake kubwa imekuwa ikitajwa ni kucheza Barcelona. Mchezaji huyo amekuwa akidaiwa kuwa na mazungumzo pia na timu za Ligi kuu ya Saudia Arabia, huku kuwa na ofa kutoka Italia ambako vigogo wa soka wa nchi hiyo, Inter Milan na AC MIlan zinahusishwa naye.


Bryan Mbeumo

MSHAMBULIAJI wa Brentford, Bryan Mbeumo anataka kujiunga na Manchester United ambayo kwa sasa inajiandaa kuanza mazungumzo na timu yake kwa ajili ya kumsajili katika dirisha hili la usajili. Mbeumo ambaye msimu uliopita alicheza mechi 42 za michuano yote na kufunga mabao 20, anaweza kuuzwa kwa kiasi kisichopungua Pauni 50 milioni.


Rasmus Hojlund

INTER Milan inatarajia kumsaini kwa mkopo mshambuliaji wa Manchester United na Denmark, Rasmus Hojlund, 22, katika dirisha hili. Hojlund ni miongoni mwa mastaa ambao hawakuwa wanapata nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Man United na yupo tayari kuondoka kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine.


Myles Lewis-Skelly

BEKI wa Arsenal, Myles Lewis-Skelly, 18, anatarajiwa kusaini mkataba mpya katika dirisha hili baada ya siku kadhaa tangu kuibuka kwa ripoti kwamba yupo katika rada za Real Madrid iliyopanga kumsajili katika dirisha hili pia. Beki huyo anaonekana kuwa ni hazina kubwa Arsenal na msimu uliomalizika alicheza mechi 42 za michuano yote.


Jean-Philippe Mateta

MSHAMBULIAJI wa Ufaransa na Crystal Palace, Jean-Philippe Mateta, 27, pia yupo kwenye orodha ya wachezaji ambao Manchester United inataka kuwasajili katika dirisha hili kwa ajili ya kuboresha eneo la ushambuliaji ambalo lilikuwa na upungufu mkubwa katika msimu uliopita. Mkataba wa Mateta unatarajiwa kumalizika 2026.


Jamie Gittens

MABOSI wa Chelsea wapo tayari kulipa Pauni 50 milioni kwenda Borussia Dortmund kwa ajili ya kumsajili winga wa timu hiyo na timu ya taifa ya England, Jamie Gittens katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kuvutiwa na kiwango alichoonyesga msimu uliopita. Gittens mwenye umri wa miaka 20, msimu uliomalizika alicheza mechi 48 za michuano yote Ujerumani na Ulaya na kufunga mabao 12.


Aleksandar Mitrovic

EVERTON, Manchester United na West Ham United zinataka kuingia vitani kwa ajili ya kupambania kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Serbia, Aleksandar Mitrovic anayeichezea Al-Hilal ya Saudia Arabia katika dirisha hili. Taarifa zinaeleza kwamba mabosi wa Al-Hilal wapo tayari kumruhusu mchezaji huyo kuondoka ikiwa atalazimisha kufanya hivyo.


Jarrad Branthwaite

CHELSEA inataka kumsajili beki wa kati wa Everton na England, Jarrad Branthwaite, 22, lakini inatarajiwa kukumbana na upinzani mkubwa kutoka kwa  Tottenham Hotspur ambayo pia inahitaji saini yake. Branthwaite ambaye msimu uliomalizika alicheza mechi 33 za michuano yote huko England,mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2027.