Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Van Nistelrooy atimua wawili benchi

Van Pict

Muktasari:

  • Leicester City kwa sasa inashika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, pointi tano kufika kwenye eneo salama. Kichapo cha mabao 4-0 mbele ya mashabiki wao kutoka kwa Brentford kimezidisha hofu zaidi ya mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu England kushuka daraja.

LEICESTER, ENGLAND: LEICESTER City imewafuta kazi makocha wawili wa kikosi cha kwanza baada ya sasa timu hiyo kuwa kwenye presha kubwa ya kushuka daraja kutokana na matokeo ya hovyo uwanjani.

Leicester City kwa sasa inashika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, pointi tano kufika kwenye eneo salama. Kichapo cha mabao 4-0 mbele ya mashabiki wao kutoka kwa Brentford kimezidisha hofu zaidi ya mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu England kushuka daraja.

Ushindi kwa timu za West Ham na Wolves katika mechi zao za wikiendi iliyopita dhidi ya Arsenal na Bournemouth mtawalia, hilo limeifanya timu hiyo ya Kocha  Ruud van Nistelrooy kuwa kwenye hatari zaidi.

Katika kufanya mambo yanabadilika kwenye timu, mabosi wa Leicester City wameamua kuwafuta kazi wakocha wawili kwenye benchi la ufundi huku hilo likidaiwa ni uamuzi wa kocha mkuu Van Nistelrooy.

Makocha hao wawili wa kikosi cha kwanza waliofutwa kazi ni Ben Dawson na yule wa makipa Danny Alcock.

Taarifa ya klabu hiyo ilisomeka: “Leicester City imeachana na makocha wa kikosi cha kwanza Ben Dawson na Danny Alcock. Wote Ben na Danny walijiunga na timu yetu mwanzoni mwa msimu 2024/25, walifanya kazi na Steve Cooper na Ruud van Nistelrooy na walikuwa pia makocha wa muda kwenye kikosi hicho cha kwanza.

“Tunawashukuru Ben na Danny kwa mchango wao na tunawatakia kila la heri kwenye maisha yao.”

Leicester City ilimteua Van Nistelrooy kuwa meneja wao mwishoni mwa Novemba mwaka jana baada ya kumfuta kazi Steve Cooper. Mechi yake ya kwanza aliwakabili West Ham, Desemba 3, alishinda 3-1, kabla ya kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Brighton siku tano baadaye. Lakini, Leicester City baadaye ilicheza mechi saba na kupoteza, huku ushindi wao pekee ulikuwa mbele ya Tottenham iliyokuwa na majeruhi kibao.

Hata hivyo, baadaye ilirudi tena kwenye mechi za vichapo, ilipotandikwa 4-0 na Everton kabla ya kupigwa 2-0 na Arsenal na 4-0 dhidi ya Brentford. Kipigo hicho cha mwisho kilichowakuta Ijumaa, Leicester City iliweka rekodi ya hovyo, ya kuwa timu ya kwanza kwenye Ligi Kuu England kupoteza mechi sita mfululizo za nyumbani bila ya kufunga bao lolote, huku ikiruhusu mabao 15.

Leicester City mechi yao ijayo watakwenda ugenini kukipiga na West Ham kabla ya kukabiliana na ratiba ngumu sana dhidi ya Chelsea, Manchester United, Manchester City na Newcastle United.