Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Valverde aanika Arsenal ilivyomkosa

Valvede Pict
Valvede Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo amefichua aliipa kipaumbele Arsenal akitamani kujiunga nayo hadi kufikia majaribio pindi alipokuwa kijana mdogo, lakini hazikuweza kutimia kwa vile hakuonekana angeweza kufiti kuchezea timu hiyo.

MADRID, HISPANIA: UKIONA cha nini, wenzako wanajiuliza watakipata lini na hicho ndicho pengine kinaitokea Arsenal inapomtazama kiungo wa Real Madrid na Uruguay, Federico Valverde.

Mchezaji huyo amefichua aliipa kipaumbele Arsenal akitamani kujiunga nayo hadi kufikia majaribio pindi alipokuwa kijana mdogo, lakini hazikuweza kutimia kwa vile hakuonekana angeweza kufiti kuchezea timu hiyo.

Baada ya hapo, Valverde alitimkia Real Madrid ambako alipata fursa ya kujiunga na kikosi cha vijana cha miamba hiyo ya Hispania na Ulaya hadi kufikia kuwa miongoni mwa wachezaji wake tegemeo na waliopata mafanikio makubwa kwa miaka nane (8) aliyoitumikia.

Tangu alipopewa nafasi kwa mara ya kwanza katika kikosi cha wakubwa cha Real Madrid, Valverde amekuwa tegemeo la timu hiyo huku akifanikiwa kutwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na matatu ya Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’.

Hata hivyo, stori ya Valverde leo ingekuwa tofauti kama Arsenal ingetumia fursa ya kumsajili miaka 10 iliyopita wakati huo ilipokuwa ikinolewa na Kocha Arsene Wenger.

Mchezaji huyo alialikwa kufanya majaribio ya wiki moja na kikosi cha kwanza cha Arsenal na alipata fursa ya kucheza sambambamba na mastaa wa timu hiyo wakati huo kama Santi Cazorla na Alexis Sanchez lakini hakuweza kumshawishi Wenger kumsajili.

“Nilikuwa na umri wa miaka 16, ndivyo ilivyokuwa, hii ni klabu yangu. Nitakulia hapa (Arsenal). Ligi Kuu England (EPL) inatazamwa sana kule Uruguay. Niliwaza wakati ujao nikiwa pale. Niliifurahia na kufanya mazoezi na wachezaji wa kipekee,” alisema Valverde katika mahojiano yake na jarida la Marca.

Valverde amefichua changamoto kubwa katika majaribio yake ilikuwa ni lugha na mchezaji aliyempa usaidizi wa karibu katika kipindi cha majaribio yake ndani ya Arsenal alikuwa ni kipa anayedakia Aston Villa kwa sasa, Emiliano Martinez.

“Sijui Kiingereza na walilazimika kunielezea kila kazi. Sijui kama ananikumbuka lakini Dibu (Martinez) alikuwa mmoja kati ya walionisaidia sana kwa kila kitu wengine wakiwa ni Bellerin (Hector), Alexis (Sanchez) na Cazorla (Santi).

“Nilikuwa tayari nimeshashindana na watu wakubwa katika Ligi Kuu ya Uruguay. Nilihisi nilikuwa tayari kwa hatua kubwa.

Baada ya hilo la kujiunga na Arsenal kushindikana, Valverde alitua Real Madrid ambayo hadi sasa ameshaichezea zaidi ya mechi 200 na kando yake wakiwepo mastaa wakubwa kama Vinicius Junior, Kylian Mbappe, Jude Bellingham na Rodrygo.

Wakati Valverde akitwaa mataji hayo makubwa akiwa na Real Madrid, Arsenal bado inahaha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya na tangu 2016 hadi sasa haijabeba.

Arsenal kwa sasa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi 19 ambazo ni tisa pungufu ya pointi za vinara Liverpool iliyo na pointi 28.