Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yoga na afya ya akili kwa mwanamke wa kisasa

Muktasari:

  • Utamkuta anafanya kazi kazini, analea familia, anahudhuria mikutano na bado anatakiwa kuhifadhi mwonekano na utulivu wake ili kusalia na uzuri wa asili.

KATIKA ulimwengu wa sasa unaokimbia kwa kasi, mwanamke wa kisasa amekuwa akibeba majukumu mengi kwa wakati mmoja.

Utamkuta anafanya kazi kazini, analea familia, anahudhuria mikutano na bado anatakiwa kuhifadhi mwonekano na utulivu wake ili kusalia na uzuri wa asili.

Ni katika mazingira haya ndipo yoga, inapoibuka si kama mtindo wa mazoezi tu, bali kama tiba ya akili, mwili na roho na njia ya kurudisha utulivu uliopotea kwenye mizunguko ya maisha ya kila siku.


MAANA YA YOGA

Mchezo wa yoga ni aina ya mazoezi ya mwili, akili na roho yanayolenga kuleta uwiano, utulivu na afya bora kwa mwili na akili.

Asili yake ni kutoka India. Neno ‘yoga’€  linatokana na lugha ya Sanskrit likimaanisha ‘umoja’ au ‘kuunganisha’, yaani kuunganisha mwili, akili na nafsi.

YOGA NA MSONGO WA MAWAZO

Msongo wa mawazo (stress) ni kati ya changamoto kubwa kwa wanawake wengi wa mijini, uchovu wa kazi, presha za kifamilia, na matarajio ya kijamii mara nyingi hujenga mzigo unaoathiri afya ya akili.

Utafiti mwingi umeonyesha kuwa kufanya yoga kwa utaratibu hupunguza kiwango cha homoni ya msongo wa mawazo, na kusaidia ubongo kupata utulivu.

Harvard Medical School (2018) -- “ Mind-Body Medicine Research

-Utafiti uliofanywa katika Harvard Medical School -- Benson-Henry Institute for Mind Body Medicine (2018), ulionyesha kuwa watu wanaofanya yoga mara tatu kwa wiki walipunguza kiwango cha cortisol kwa wastani wa asilimia 31 baada ya wiki nane.

Kupitia mbinu za kupumua kwa kina (*pranayama*), mwili huanza kujifunza kujibu kwa utulivu badala ya wasiwasi. Mwanamke anapojifunza kushikilia pumzi na kuiachia kwa makusudi, anaanza pia kujifunza kushikilia hisia na kuziachia bila maumivu. Kwa maneno mengine, yoga humfundisha mwanamke -- kupumua maisha kwa ujasiri --  hata katikati ya changamoto.

KUBORESHA USINGIZI NA UBORA WA KUPUMZIKA

Wanawake wengi wa mijini hulalamika kuhusu usingizi hafifu au mawazo yanayowazunguka usiku mzima. Mwili unapokuwa umechoka lakini akili inakimbia, usingizi hubaki ndoto.

Yoga, husaidia kutuliza mfumo wa mwili unapoingia katika hali ya kupumzika, mapigo ya moyo hupungua na akili hutulia.

Daktari wa afya ya akili, Dk. Amina Mdee, anaeleza: ”Mwanamke anayejenga utaratibu wa kufanya yoga mara tatu kwa wiki ana uwezekano mkubwa wa kupata usingizi mzuri na amani ya ndani, kwani hufanya ubongo uzalishe kemikali za serotonin na melatonin, zinazosaidia kulala na kuamka ukiwa na nguvu mpya.”


KUONGEZA KUJIAMINI, KUJIKUBALI

Moja ya zawadi kubwa ambayo yoga humletea mwanamke ni kujiamini. Wakati mazoezi mengi huzingatia mwonekano wa nje -- kupunguza tumbo au kuongeza makalio.

Mmoja kati ya Wanadada maarufu ambao wanacheza mchezo huu ambaye hakutaka jina lake kutajwa anasema; “Yoga huzingatia zaidi hisia za ndani. Mwanamke anapojifunza kusawazisha mwili wake katika pozi gumu, anajifunza pia uvumilivu, nidhamu na upendo kwa nafsi yake.”

KUUNGANISHA MWILI NA AKILI

Wengi hufikiri yoga ni mazoezi ya kunyoosha mwili pekee, lakini kiuhalisia ni falsafa ya maisha. Yoga humsaidia mwanamke kutambua uhusiano wa karibu kati ya mwili na akili.

Dk Mdee anasema: “Wakati mwili unaposikia maumivu, mara nyingi ni kielelezo cha kitu kinachoendelea ndani ya akili, kupitia meditation na indfulness, mwanamke hujifunza kusikiliza sauti ya ndani, kutambua hisia zake, na kuishi kwa utambuzi zaidi.

Mwanamke wa kisasa anaishi katika dunia ya taarifa zisizoisha simu, barua pepe, mitandao ya kijamii. Yoga humsaidia kuondoka kwenye kelele hizo na kurudi kwenye “nafasi yake safi”  ya utulivu. Hapo ndipo anapoweza kufikiri kwa uwazi, kupanga maisha kwa hekima, na kufanya uamuzi wenye busara zaidi.

KUBADILISHA MAISHA HALISI

Wapo wanawake wengi waliogeuza maisha yao kupitia yoga. Mfano, Neema Mwakalinga, mfanyakazi wa benki jijini Dar es Salaam, anasema alianza Yoga baada ya kupata ‘burnout’ (kuchoka kupita kiasi kisaikolojia na kimwili).

“Nilikuwa na maumivu ya kichwa kila siku, usingizi haukunipata, nilihisi nimelemewa. Nilipoanza yoga, mwanzoni ilikuwa ngumu, lakini sasa ni tiba yangu ya maisha. Nimejifunza kupumua, kukubali mabadiliko na kuwa na amani hata siku ngumu kazini.”

Hadithi kama ya Neema ni mfano wa jinsi yoga inavyoweza kumsaidia mwanamke kuishi kwa usawa katika dunia isiyo na usawa. Ni mwaliko wa kurudi kwenye asili ya utu na utulivu, upendo, na uwiano.


MWANAMKE MJANJA NA AFYA YA AKILI

DK Mdee anasema: “Kwa mwanamke wa kisasa, mafanikio si tu kupanda cheo kazini au kuwa mama bora, bali pia ni kuwa na akili yenye amani na moyo ulio huru.

“Yoga ni njia ya kurudisha utulivu huo, kupitia pumzi, mwili na akili huungana, na mwanamke anajikuta akitabasamu bila sababu, akiwa na nguvu mpya na mtazamo chanya.”

Kama alivyoandika mwalimu maarufu wa yoga, B.K.S. Iyengar: “Afya ni hali ya upatanisho kati ya mwili, akili na roho. Yoga ni daraja linalounganisha vyote.”€

Kama wewe ni mwanamke unayejiamini na kujipenda hii ni fursa nyingine ya kujipunguzia matatizo yasiyo ya lazima kama vile msongo wa mawazo kwa kucheza mchezo wa yoga.