Ulinzi wa Uefa sio mchezo

Muktasari:
- Mbali ya operesheni zilizofanyika katika Jiji la Munich, pia kuna ulinzi mkali huko jijini Paris ambako askari wakijiandaa na vurugu zitakazotokea ikiwa PSG itashinda au kufungwa.
PARIS, UFARANSA: OPERESHENI kubwa ya usalama yenye polisi wa kutuliza ghasia na ulinzi mkali iliandaliwa nchini Ufaransa kabla ya mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya PSG na Inter Milan itakayo pigwa baadae huko Munich, Ujerumani.
Mbali ya operesheni zilizofanyika katika Jiji la Munich, pia kuna ulinzi mkali huko jijini Paris ambako askari wakijiandaa na vurugu zitakazotokea ikiwa PSG itashinda au kufungwa.
Jiji la Paris lilituma maafisa wa polisi 5,400 kufanya doria maeneo mbalimbali ya Jiji hilo kwa ajili ya mechi ya mechoi hiyo.
Mkuu wa polisi jijini Paris, Laurent Nunez alisema licha ya mechi hiyo kuchezwa mjini Munich, matokeo yake yalitarajiwa kusababisha sherehe jijini Paris au vurugu katika jiji la Paris.
Polisi wanaamini kungekuwa na vurugu kama zile zilizozuka mitaani saa chache baada ya mechi ya nusu fainali kati ya PSG na Arsenal.
Kukabiliana na hilo, vikosi vya polisi vilitumwa kwenda kuongea nguvu huko Paris ambapo askari wengi walikuwa wakilinda maeneo mbalimbali ya mji, hasa katika barabara ya Champs-Elysees, ambako mashabiki wana tabia ya kujaa ikiwa PSG imepata matokeo mazuri.
Polisi pia walifunga barabara karibu na eneo hilo, na waliongeza wingi wa kamera na kufuatilia matukio yaliyoendelea eneo hilo kwa umakini wa hali ya juu.
Usalama pia uliimarishwa katika uwanja wa Parc des Princes, ambao ni uwanja wa nyumbani wa PSG ulioko pembezoni mwa jiji upande wa kusini-magharibi.
"Tuna mtandao mkubwa kote katika eneo la jiji. kutakuwa na ulinzi mkubwa katika mji mkuu na maeneo ya jirani kwa ujumla kutakuwa na askari 5,400,"alisema Mkuu wa Polisi jijini humo.
"Tumewaita wafanyakazi kutoka makao makuu ya polisi, na Waziri wa Nchi ametuwekea vikosi vingi vya kuhamahama, CRS (polisi wa kutuliza ghasia)."
Video za kushtusha kutoka zilizorekodiwa saa chache baada ya mechi ya PSG dhidi ya Arsenal zilionyesha gari likiwagonga mashabiki kabla ya kuchomwa moto.
Magofu ya gari hilo lililochomwa yalionekana kwenye barabara ya Rue Christophe-Colomb, karibu na Champs-Élysees ambako vijana mashabiki wa PSG walionekana wakikabiliana na polisi wa kutuliza ghasia.
Kulikuwepo taarifa kuwa baadhi yao walivamia maduka na mabenki, wakivunja madirisha.
Msemaji wa Idara ya Polisi ya Paris alisema kuwa angalau watu 43 walikamatwa wakati wa sherehe za ushindi wa PSG kwa kosa kosa ya kuvuruga amani.
Wakati huo huo, polisi katika jiji mwenyeji la Munich pia walijiandaa kwa mechi hii ya fainali iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu.
Idadi kubwa ya polisi ilionekana kote jijini humo, zaidi ya maaskari 2,000 wa usalama walikuwepo maeneo muhimu.
Hii ni pamoja na uwanjani Allianz Arena, ambako mechi ilichezwa, na maeneo ambayo maelfu ya mashabiki walikusanyika kwa ajili ya kutazama mechi hiyo kwa pamoja bila malipo.
Kabla ya mechi, Msemaji wa polisi wa Ujerumani alisema: "Tunatarajia watu wenye vurugu watakuwepo. Lakini tumejiandaa vizuri. Mashabiki wa Italia ndio wanaonekana kuwa na hali ya kuchangamka sana, kwa hiyo."
Polisi wa siri wenye walikuwepo kuzunguka uwanja na maeneo ya karibu, pia kulikuwa na vizuizi ambavyo vilizuia magari yasiyohusika kwenda eneo ambalo linaweza kuwapa uhuru wa kujeruhi mashabiki kama ilivyotokea katika sherehe za ubingwa za Liverpool ambapo gari ilijeruhi zaidi ya watu 79.