Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uhondo wa Kombe la Dunia la Klabu upo hivi

UHONDO Pict

Muktasari:

  • Tangu 2005, ambapo michuano hiyo ilikuwa ikifanyika kila mwaka inapofika Desemba, hadi hapo 2023 Fifa ilipothibitisha kwamba Marekani itaandaa michuano hiyo ambayo itafahamika kama Kombe la Dunia la Klabu, ambapo itakuwa utangulizi kabla ya fainali za Kombe la Dunia 2026.

LOS ANGELES, MAREKANI: FAINALI za Fifa za Kombe la Dunia la Klabu 2025 ni michuano ya 21, lakini safari hii itafanyika kwa mtindo tofauti kama ilivyokuwa kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliomalizika wa 2024/25.

Tangu 2005, ambapo michuano hiyo ilikuwa ikifanyika kila mwaka inapofika Desemba, hadi hapo 2023 Fifa ilipothibitisha kwamba Marekani itaandaa michuano hiyo ambayo itafahamika kama Kombe la Dunia la Klabu, ambapo itakuwa utangulizi kabla ya fainali za Kombe la Dunia 2026.

Michuano hiyo itafanyika kwenye viwanja kadhaa huko Marekani, itaanza Juni 14 hadi Julai 13, ambapo timu 32 zilichaguliwa kutokana na viwango kwenye ligi za nchi husika. Michuano hiyo itashirikisha vigogo wa maana.

Jambo hilo linafanya fainali za Kombe la Dunia la Klabu kuwa lenye mvuto mkubwa kulitazama. Awali michuano hiyo ilikuwa ya timu saba, lakini sasa ni 32 zilizogawanywa kwenye makundi manane yenye timu nne. Baada ya hatua ya makundi kutakuwa na mtoano wa hatua ya 16 bora, robo fainali, nusu fainali na hatimaye fainali.

UHO 02

Makundi yalivyo

Kundi A: Palmeiras, FC Porto, Al Ahly, Inter Miami

Kundi B: Paris St-Germain, Atletico Madrid, Botafogo, Seattle Sounders

Kundi C: Bayern Munich, Auckland City, Boca Juniors, Benfica

Kundi D: Flamengo, Esperance Sportive de Tunisie, Chelsea, Los Angeles FC

Kundi E: River Plate, Urawa Red Diamonds, Monterrey, Inter Milan

Kundi F: Fluminense, Borussia Dortmund, Ulsan, Mamelodi Sundowns

Kundi G: Manchester City, Wydad, Al Ain, Juventus

Kundi H: Real Madrid, Al Hilal, Pachuca, Salzburg.

Timu hizo zimechaguliwa kutoka katika mashirikisho sita tofauti na itafanyika kila baada ya miaka minne. Kuna timu za kutoka Asia (ACF), Afrika (CAF) na Amerika Kaskazini na Kati na Caribbean (CONCACAF) ambapo kila moja imetoa timu nne, wakati CONMEBOL, ambayo ni Amerika Kusini imetoa timu sita, huku UEFA ikitoa timu 12. Shirikisho la OFC limetoa timu moja ambayo ni Auckland City inayowakilisha Oceania. Kufikia idadi ya timu 32, mwenyeji amepewa nafasi moja ya ziada na ndipo hapo timu ya Inter Miami ilipopata nafasi ya kuchaguliwa kushiriki.

Kilichozingatiwa kwa timu zilizochaguliwa kushiriki fainali hizo ni zile zilizofanya vizuri kwenye mashirikisho yake kati ya mwaka 2021 na 2024.

Wakati mashabiki wa soka wakisubiri kwa hamu kuanza kwa fainali hizo kitu kizuri ni kwamba zitarushwa mubashara bure kabisa katika lugha 14 tofauti kupitia DAZN, mtandao unaorusha matangazo ya michezo duniani ambapo utakuwa na jukumu la kuonyesha moja kwa moja mechi zote 63 za michuano hiyo. Na si tu kuonyesha mubashara mechi 63, DAZN pia itakuwa na kazi ya kuonyesha marudiano ya mechi hizo na mambo mengine ili kuhakikisha mashabiki wanaburuka na kupata ladha zote za michuano hiyo.

Mechi ya kwanza ya michuano hiyo itapigwa Juni 14 wakati fainali itapigwa kwenye Uwanja wa MetLife mjini New Jersey, Julai 13. Mechi ya kwanza itashuhudia kikosi cha supastaa Lionel Messi, Inter Miami kukipiga na miamba ya soka ya Afrika, Al-Ahly kwenye Uwanja wa Hard Rock.

Timu vigogo kama Real Madrid na Bayern Munich ni miongoni mwa timu zitakazoiwakilisha UEFA baada ya kukosekana kwa miamba mingine kama Barcelona, Arsenal na Manchester United. Kikosi cha Inter Miami kimekuwa na mvuto kutokana na timu hiyo kuwa na mastaa wa maana waliowahi kutamba Ulaya kama Messi, Luis Suarez, Sergio Busquets na Jordi Alba. Mashabiki walitamani kumshuhudia mkali Cristiano Ronaldo akishiriki pia fainali hizo, lakini timu yake ya Al Nassr haijafuzu na hakuwa tayari kuhamia timu nyingine iliyofuzu ikiwamo wapinzani wao Saudi Pro League, Al Hilal.

UHO 01

Mchanganuo

UEFA: Bayern Munich, Borussia Dortmund, Real Madrid, Manchester City, Chelsea, Inter Milan, Paris Saint-Germain, Benfica, Porto, FC Salzburg, Juventus, Atletico Madrid

CONMEBOL: Palmeiras, Flamengo, Fluminense, River Plate, Boca Juniors, Botafogo

OFC: Auckland City

CAF: Al Ahly, Wydad Casablanca, Esperance de Tunis, Mamelodi Sundowns

AFC: Al-Hilal, Urawa Red Diamonds, Al Ain, Ulsan HD

CONCACAF: Monterrey, Seattle Sounders, Club Leon, Pachuca

Wenyeji: Inter Miami

UHO 04

Mkwanja mezani

Jumla ya zawadi ya pesa kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu ni Dola 1 bilioni, huku timu itakayonyakua ubingwa itaweka kibindoni Dola 125 milioni. Nusu ya Dola 1 bilioni itawagawanya kwa timu 32, huku mgawo huo ukizingatia michezo na mambo ya kibiashara. Hiyo ina maana timu kama Man City na Real Madrid zitapata mgawo mkubwa kuliko ndogo kwa mujibu wa Fifa na Uefa. Dola 475 milioni zitagawawia kwa kuzingatia viwango uwanjani. Timu itakayoshinda mechi nyingi itakusanya mkwanja mrefu, ambapo Dola 125 milioni zitakwenda kwa bingwa atakayeshinda mechi nyingi (saba) hadi mwisho wa michuano. Hatua ya makundi itaanza Juni 14 hadi 26 wakati raundi ya 16 bora itapigwa kati ya Juni 28 na Julai 1, huku robo fainali ni Julai 4 na 5, nusu fainali ni Julai 8 na 9 na fainali itakuwa Julai 13.

UHO 03

Viwanja

MetLife Stadium (East Rutherford, New Jersey), Hard Rock Stadium (Miami, Florida), Mercedes-Benz Stadium (Atlanta, Georgia), Lumen Field (Seattle, Washington), Bank of America Stadium (Charlotte, North Carolina), TQL Stadium (Cincinnati, Ohio), Rose Bowl Stadium (Los Angeles, California), GEODIS Park (Nashville, Tennessee), Camping World Stadium (Orlando, Florida), Inter&Co Stadium (Orlando, Florida), Lincoln Financial Field (Philadelphia, Pennsylvania) na Audi Field (Washington, DC).