Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Timu ya mastaa wa nguvu Italia inavyoshushwa hadi mchangani 

MASTAA Pict

Muktasari:

  • Klabu hiyo ya Brescia sasa itaondoshwa kwenye uso wa soka la kulipwa huko Italia baada ya kutamba kwa miaka 114 kufuatia kutangazwa kuwa mufilisi.

MILAN, ITALIA: UKICHOKA, watu wanakuchoka zaidi. Ndicho unachoweza kusema juu ya stori ya klabu maarufu ya soka ya huko Italia, Brescia ambayo imeondoshwa kabisa kwenye soka la kulipwa la nchi hiyo baada ya kufilisika na kushindwa kulipa madeni yake, kiasi cha Euro 3 milioni.

Klabu hiyo ya Brescia sasa itaondoshwa kwenye uso wa soka la kulipwa huko Italia baada ya kutamba kwa miaka 114 kufuatia kutangazwa kuwa mufilisi.

Timu hiyo ambayo ilianza msimu huu kwenye Serie B - imeshindwa kulipa madeni yake yanayoripotiwa kuwa Euro 3 milioni (zaidi ya Pauni 2.5 milioni)

Kutokana na kuwa mufilisi, timu hiyo imekabiliwa na sakata la kuondolewa kwenye ligi za soka la kulipwa na badala yake inakuwa klabu ya mchangani.


NINI KIMEWAKUTA?

Brescia siku za karibuni ilikuwa ikicheza kwenye ligi ya ngazi ya pili huko Italia, Serie B na ilinusurika kidogo kushuka daraja. Wengi waliamini ingeendelea kubaki kwenye ligi hiyo hadi msimu ujao. Na kwenye mchakato wa ligi hiyo, walipokwa pointi nne kutokana na kuwa na ukata, ambapo ungewafanya washuke hadi kwenye Serie C. Hata hivyo, baada ya kushindwa kulipa madeni yao yanayofikia Euro 3 milioni, klabu hiyo yenye umri wa miaka 114 sasa itaondoshwa kwenye ligi zote za soka la kulipwa huko Italia.


UKUBWA WA TATIZO

Brescia inamilikiwa na Massimo Cellino - ambaye alikuwa bosi wa Leeds United kadi ya 2014 na 2017 kabla ya kwenda kuinunua klabu hiyo ya Italia. Lakini, sasa timu hiyo ilitakiwa hadi kufika Ijumaa iliyopita kulipa mishahara yote ya miezi miwili iliyopita, ambayo ilikuwa ikidaiwa. Hata hivyo, siku hiyo ilipita bila ya malipo yoyote kufanyika. Tangu 2017, Biancazzurri ilikuwa ikimilikiwa na Massimo Cellino, ambaye ni mjasiliamali wa Kitaaliano. Cellino aliwahi kuimiliki Leeds United, ambaye alikuwa na matatizo mengi na kuiweka klabu hiyo kwenye mikwamo mikubwa ya kiuchumi.


KITU UNACHOPASWA KUJUA

Kuondoshwa kwa Brescia kwenye soka la kulipwa kunaleta athari kubwa kwenye maisha ya mastaa wakubwa na waliopata umaarufu mkubwa kwenye soka, kiasi kwamba kama wanaamua kuchanga kulipa deni hilo, basi timu hiyo inabaki kwenye ramani ya soka la kulipwa.

Kuna mastaa kibao wenye majina makubwa waliwahi kuchezea timu hiyo akiwamo Roberto Baggio, Pep Guardiola, Andrea Pirlo, Luca Toni, Sandro Tonali, Marek Hamsik, Roberto De Zerbi na hivi karibuni Super Mario Balotelli. Balotelli aliitumikia timu hiyo kwa mwaka mmoja, wakati aliposajiliwa mwaka 2019 - alifunga mabao matano katika mechi 19, lakini aliondoka baada ya timu kushuka daraja.

Brescia ilipanda daraja na kucheza Serie A mwaka 2019, lakini ilishuka daraja msimu uliofuata. Na mambo yaliendelea kuwa mabaya zaidi msimu huu, ambapo kitendo cha kukatwa pointi nne kutokana na ukata wa kiuchumi, kilikuwa kinawafanya kushuka hadi kwenye Serie C.

Brescia si timu pekee kwenye soka la Italia ambayo ilitangazwa mufilisi na kuondolewa kwenye ligi za soka la kulipwa. Spal, ambayo iliyowahi kucheza Serie A, nayo iliwahi kukumbwa na sakata kama hilo.


KIPI KINAWASUBIRI BRESCIA?

Kutokana na hilo, timu hiyo sasa itashushwa madaraja hadi Serie D, ligi ya chini zaidi kwenye soka la Italia isiyokuwa ya kulipwa. Na timu hiyo ipo kwenye hatari ya kufutika kabisa kama hakutakuwa na tajiri mpya wa kuja kuinunua na bosi wao wa sasa Cellino akipelekwa mahakamani kutangazwa mufilisi.