Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spurs yapindua meza kwa Marc Guehi

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Mkataba wake na Crystal Palace unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na Spurs inafanya mazungumzo ili kumsajili kama mchezaji huru. Mbali ya Tottenham, staa huyo pia anahusishwa na Liverpool na Real Madrid, lakini taarifa za hivi karibuni zinadai kwamba Spurs ina nafasi nzuri ya kumchukua.

TOTTENHAM Hotspur inatajwa kuwa miongoni mwa timu zinazofanya mazungumzo kwa ajili ya kuipata saini ya beki kisiki wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Marc Guehi, mwenye umri wa miaka 25.

Mkataba wake na Crystal Palace unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na Spurs inafanya mazungumzo ili kumsajili kama mchezaji huru. Mbali ya Tottenham, staa huyo pia anahusishwa na Liverpool na Real Madrid, lakini taarifa za hivi karibuni zinadai kwamba Spurs ina nafasi nzuri ya kumchukua.

Mabosi wa Crystal Palace wanajaribu kufanya mazungumzo ili kumsainisha mkataba mpya kwa sababu hawataki akiondoka bure, lakini hadi sasa mpango huo umefeli kwani Guehi mwenyewe hataki.

Mchezaji huyo alikuwa karibu kujiunga na Liverpool katika dirisha lililopita kabla ya mambo kubadilika dakika za mwisho na dili kufeli. Siku kadhaa zilizopita, taarifa mpya zilieleza kwamba Guehi aliwaambia wawakilishi wake kwamba anahitaji kujiunga na Real Madrid ambayo imeonyesha nia ya kumchukua Januari.

Tangu kuanza kwa msimu huu, staa huyo ambaye pia ni nahodha wa Palace amecheza mechi 10 za michuano yote.


Nathan Collins

KOCHA wa Tottenham Hotspur, Thomas Frank amependekeza jina la beki wa kati wa Brentford, Nathan Collins ambaye aliwahi kumfundisha. Brentford inaripotiwa kuwa tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 katika dirisha lijalo la Januari ingawa ni kwa ada ya uhamisho inayoweza kufika Pauni 40 milioni. Kocha huyo ameona kuna upungufu katika safu ya ulinzi na anaamini Collins ndiye tiba ya tatizo hilo.


Rodrigo Bentancur

KIUNGO wa Tottenham Hotspur, Rodrigo Bentancur mwenye umri wa miaka 28, yupo karibu kusaini mkataba mpya na klabu hiyo baada ya kufikia makubaliano hivi karibuni. Kocha Thomas Frank aliwaambia vigogo wa Spurs kwamba anahitaji uwepo wa Bentancur katika kikosi chake kutokana na mchango wake. Awali, vigogo wengine Ulaya ikiwemo Real Madrid walikuwa wakihusishwa na mpango wa kutaka kumsajili.


Federico Valverde

KIUNGO wa Real Madrid, Federico Valverde, 27, ameingia katika rada za Manchester United ambayo inaripotiwa kuwa tayari kutoa Euro 80 milioni kwa ajili ya kumsajili. Mkataba wake na Real Madrid unamalizika 2029, lakini timu yake hiyo ya Hispania inaweza kuwa tayari kumuuza ikiwa timu inayomhitaji itawasilisha ofa nzuri. Kwa sasa mazungumzo bado yanaendelea na Man United inatazamia kumsajili mwisho wa msimu hata kama ni kwa mkopo kama ikishindwa kumnunua mazima.


Hayden Hackney

FULHAM inapanga kumsajili kiungo wa Middlesbrough, Hayden Hackney mwenye umri wa miaka 23 katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Hackney ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Middlesbrough na inadaiwa kuhitaji kiasi kisichopungua Pauni 20 milioni ili kumuuza. Mkataba wa sasa wa staa huyo unatarajiwa kumalizika 2027 na msimu uliopita alicheza mechi tisa za michuano yote.


Almugera Kabar

BRENTFORD imeendela kufanya mazungumzo ya kumsajili beki wa pembeni wa Borussia Dortmund, Almugera Kabar mwenye umri wa miaka 19. Staa huyo wa kimataifa wa Ujerumani ni miongoni mwa vijana waliopandishwa kutoka akademi ya Dortmund na amewahi kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani kwa vijana wenye umri chini ya miaka 19. Kabar anaweza kucheza nafasi za beki wa kulia na kushoto, na sehemu ya ubora wake ni kupandisha mashambulizi.


Jorthy Mokio

MASKAUTI wa Arsenal, Chelsea, Manchester United, Barcelona na Real Madrid zinaendelea kumfuatilia kiungo wa Ajax, Jorthy Mokio mwenye umri wa miaka 17. Staa huyo Mbelgiji ni miongoni mwa vipaji vilivyoibuka katika Ligi Kuu Uholanzi tangu msimu uliopita. Ajax inadaiwa kuhitaji zaidi ya Pauni 20 milioni ili kumuuza katika dirisha dogo la majira ya baridi.


Marc Bernal

CHELSEA inaonekana kuwa katika hatua nzuri kwenye harakati za kumsajili kiungo wa Barcelona na timu ya taifa ya vijana ya Hispania, Marc Bernal, 18, kuelekea dirisha lijalo baada ya kushindwa kumsajili katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi. Licha ya Barca kuwa tayari kumuuza staa huyo dirisha lililopita ilishindikana kutokana na majeraha aliyokuwa nayo.