Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SIO KINYONGE: Hawa wamehusika kwenye mabao mengi mwaka 2024

Muktasari:

  • Hiyo huwafanya kuhusika katika mabao mengi ya timu ukijumlisha yale waliyofunga na kusaidia wenzao kufunga kwa kuwapa pasi za mwisho.

LIVERPOOL, ENGLAND: WASHAMBULIAJI wengi wanapenda kufunga ingawa kuna wakati pia huwa wanajikita katika kusaidia wachezaji wenzao kufanya hivyo.

Hiyo huwafanya kuhusika katika mabao mengi ya timu ukijumlisha yale waliyofunga na kusaidia wenzao kufunga kwa kuwapa pasi za mwisho.

Leo, tumekuletea wachezaji watano ambao wamehusika katika mabao mengi zaidi kwa mwaka 2024, kuanzia Januari 01 hadi Desemba 31.


Robert Lewandowski (46)

Staa huyu wa kimataifa wa Poland licha ya umri kumtupa mkono anaonekana kuendelea kuwa bora siku hadi siku na msimu huu ndio anaongoza katika mbio za ufungaji bora kwenye Ligi Kuu Hispania, akiwa na mabao 16 aliyopata katika mechi 18.

Mwaka jana pia aliweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyehusika katika mabao mengi zaidi (46) kuliko wengine ambapo mabao 27 na asisti sita ilikuwa ni kwenye La Liga, mabao tisa katika Ligi ya Mabingwa, mabao mawili kwenye Copa del Rey na mawili kwenye Spanish Super Cup.


4. Vinicius Junior (46)

Vinicius tangu kuanza kwa msimu huu ndio mfungaji kinara namba mbili wa Real Madrid akiwa na mabao manane nyuma ya Kylian Mbappe mwenye mabao 10.

Kwa mwaka jana alihusika katika mabao 46, ambapo 19 ilikuwa ni ya La liga, kisha akatoa asisti tisa pia katika ligi hiyo, akafunga mabao tisa na kutoa asisti tatu katika Ligi ya Mabingwa, mabao matatu katika Spanish Super Cup,  asisti moja kwenye European Super Cup, pia ametoa asisti na kufunga bao katika FIFA Intercontinental Cup.


3. Kylian Mbappe (49)

Jumla ya mabao haya ni yale aliyofunga akiwa na PSG  na Real Madrid kuanzia Januari mwaka jana.

Akiwa na mabingwa wa Ufaransa alifunga mabao 23 na kutoa asisti nane kwenye michuano yote na katika kikosi cha Real Madrid hadi mwaka unamalizika alikuwa amefunga mabao 14 na asisti nne.

Alipokuwa na PSG, mabao tisa na asisti tano ilikuwa ni katika Ligue 1, mabao manane na asisti tatu katika Coupe de France, pia alifunga bao moja kwenye  French Super Cup.

Kwenye kikosi cha Madrid, amefunga mabao 10 na kutoa asisti 2 katika La Liga, mabao saba na asisti moja katika Ligi ya Mabingwa, pia alifunga bao katika European Super Cup, na asisti moja na bao kwenye FIFA Intercontinental Cup.


2. Harry Kane (50)

Kane ambaye msimu uliopita ndio alikuwa mfungaji bora wa Bundesliga akiwa na Bayern Munich, kwa mwaka 2024, alifunga jumla ya mabao 29 na kutoa asisti manane katika ligi hiyo, pia alifunga mabao tisa na kutoa asisti mbili katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Vilevile alifunga bao moja na asisti moja katika kombe la  DFB-Pokal.


1. Mo Salah (52)

Huyu ndio anashika namba moja katika orodha hii. Salah ambaye msimu uliopita alimaliza na mabao 18 kwenye Ligi Kuu England amekuwa kinara kutokana na mchango wake mkubwa aliouonyesha kwa msimu huu.

Kijumla kwa mwaka 2024, alifunga mabao 23 na kutoa asisti 16 katika EPL, kisha akafunga mabao mawili na asisti nne katika Ligi ya Mabingwa, mabao mawili na asisti tatu katika Europa League, pia amefunga bao moja moja katika FA na Carabao Cup.