Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sheria, teknolojia mpya kupamba Kombe la Dunia la Klabu

SHERIA Pict

Muktasari:

  • Fifa imefanya uamuzi wa kuleta mapinduzi makubwa ya kisheria kwenye fainali hizo baada ya kukubaliana na International FA Board katika kikao kilichofanyika Belfast, Februari mwaka huu.

LONDON, ENGLAND: SHERIA mpya na teknolojia mpya inafanya fainali za Kombe la Dunia za Klabu kuwa na mvuto tofauti kabisa kisoka tofauti na ilivyokuwa imezoeleka miaka ya nyuma.

Fifa imefanya uamuzi wa kuleta mapinduzi makubwa ya kisheria kwenye fainali hizo baada ya kukubaliana na International FA Board katika kikao kilichofanyika Belfast, Februari mwaka huu.

Hiyo ina maana zile sekunde tano zitaanza kuhesabiwa ambapo mwamuzi wa mchezo atanyayua mkono wake juu kuashiria kipa anapaswa kuachia mpira uliopo kwenye mikono yake ili uchezwe la ataadhibiwa kwa timu pinzani kupewa mpira wa kona.

Baada ya kushuhudia majaribio yaliofanyika kwenye mechi ya michuano ya Copa Libertadores na Copa Sudamericana, ilishuhudia matukio mawili yaliyotokana na makipa kubaki na mpira kwa muda uliozidi sekunde nane na hivyo timu pinzani kupewa faida ya mpigo wa kona.

Sheria hiyo mpya itaanza kutumika kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia la Klabu na hivyo kuwaweka makipa kwenye wakati mgumu wa kuhakikisha mipira haibaki kwenye himaya yao kwa muda mrefu na hiyo ni tiba tosha kwa makipa wenye kawaida ya kupoteza muda.

Fifa pia itatambulisha sheria nyingine ya kuwataka manahodha wa timu ndiyo watakaokuwa na ruhusu ya kuzungumza na mwamuzi ndani ya uwanja na kadi za njano zitatolewa kwa mchezaji mwingine asiyekuwa nahodha atakapokaidi na kuzungumza na refa ndani ya uwanja.

SHERI 03

Hilo pia linakwenda kukomesha wachezaji wenye kawaida ya kuwasogelea waamuzi na kuanza kuwaongelesha pindi linapokuwa tukio lenye utata mchezoni.

Kuna sheria nyingine mpya iliyopachikwa jina la ‘Arteta rule’, ikiwa na maana kutakuwa na adhabu ya kuruhusu pigo huru kwa timu yake endapo kama kocha au mchezaji wa akiba kwenye mechi kuzuia mpira uliokuwa ukitoka nje ya uwanja kabla ya kutoka wote.

Kumekuwa na kawaida ya makocha kuwahi mpira uliokuwa ukitoka nje na kuuzuia kabla ya kuvuka mstari wa mwisho wa uwanja.

Ukifanya hivyo kwa sasa ni kocha na timu pinzani itakuwa na faida ya kuwa na pigo huru dhidi ya timu yako.

Kutakuwa na sheria mpya pia ya kuhusu mapigo ya penalti na endapo kama mchezaji anayepiga mkwaju wa penalti ikitokea kwa bahati mbaya amegusa mpira mara mbili - atatakiwa kurudia pigo hilo endapo kama mpira umetinga kwenye nyavu, tofauti na awali na bao lilikuwa kikikataliwa na penalti hairudiwi.

Tukio kama hilo lilitokea kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, baina ya Atletico Madrid na Real Madrid na mchezaji Julian Alvarez, ambaye alifunga mkwaju wake wa penalti ulifutwa baada ya kuonekana amegusa mpira mara mbili na hivyo kuipa faida Los Blancos.

SHERI 02

Kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu, likitokea hilo, mchezaji atarudia kupiga mkwaju wake.

Ukiweka kando sheria mpya zitakazotumika kwenye fainali hizo, kutakuwa na mapinduzi makubwa upande wa teknolojia pia na Fifa imeweka wazi itazitumia huko Marekani.

Teknolojia kubwa kabisa itakayotumika ni ile inayotumia msaada wa Akili Mnemba inayohusu tukio la kuotea na sasa mchezaji atakapozidi kwa inchi nne, ujumbe maalumu utatumwa kwa mwamuzi msaidizi ili kunyanyua kibendera kuna tukio la mchezaji kuzidi.

Sambamba na hilo, kwa mashabiki wa mchezo wa Rugby imekuwa kawaida kuwaona waamuzi wakiwa wamefungwa kamera kwenye vifua vyao, hivyo kwenye mchezo wa soka katika fainali za Kombe la Dunia la Klabu 2025, waamuzi nao wataonekana wakiwa na kamera vifuani.

Ifab inayosimamia mabadiliko yote ya kisheria na teknolojia kwenye soka, ianze kutumika kwa kamera hizo za vifuani kwa waamuzi ili kuleta mawasiliano vizuri na skrini za VAR.

Kamera hizo zitabeba matukio pia ya matukio na mabao yatakayofungwa ndani ya uwanja moja kwa moja kwa ajili ya mashabiki waliopo nyumbani na wale waliopo uwanjani kuona kupitia skrini za televisheni zilizopo kwenye viwanja.

SHERI 01

Mazungumzo ya waamuzi wa uwanjani na wale waliopo kwenye VAR yataendelea kuonyesha hata baada ya mechi kumalizika na kwa mashabiki watakaokuwa uwanjani wataona matukio hayo kwenye televisheni za uwanjani.

Hata kwa makocha wanaotaka kufanya mabadiliko ya wachezaji kwa maana ya kutoa na kuingiza, makocha wote wa timu watakabidhiwa tablet, ambazo watatumia kuandika majina ya wachezaji inaotaka kuwatoa na wale wanaotaka waingia na kutuma majina hayo moja kwa moja kwa waamuzi wa akiba tofauti na ilivyokuwa zamani ya kuandika kikaratasi kwa waamuzi hao kuwaeleza kwamba wanataka kufanya mabadiliko ya wachezaji.