Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo rekodi zamiminika tu, sikia hii

RONALDO Pict

Muktasari:

  • Katika mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa Ureno kushinda mabao 2-1, Ronaldo alifunga bao la ushindi ambalo linamfanya kuvunja rekodi ya mabao mengi zaidi katika msimu mmoja wa Nations League A, akiwa na mabao saba.

MUNICH, UJERUMANI: JANA Cristiano Ronaldo aliiongoza Ureno kushinda mechi ya nusu fainali ya Nations League dhidi ya Ujerumani na kumwezesha kuweka rekodi mbalimbali.

Katika mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa Ureno kushinda mabao 2-1, Ronaldo alifunga bao la ushindi ambalo linamfanya kuvunja rekodi ya mabao mengi zaidi katika msimu mmoja wa Nations League A, akiwa na mabao saba.

Mabao hayo saba yanaivuka idadi iliyowahi kufungwa na waliokuwa wakishikilia rekodi hiyo ambao ni Romelu Lukaku na Ferran Torres waliofunga mabao sita msimu wa 2021/2022.

Hata hivyo, hayo ni mabao matatu pungufu ya yale aliyofunga Viktor Gyokeres alipoiwezesha Sweden kupanda kutoka Nations League C mwaka huu.

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa Ureno kufika fainali ya Nations League. Walishinda kwa mara ya kwanza mwaka 2019.

Matokeo hayo pia yalikuwa yanaweka rekodi ya ushindi wa kwanza kwa timu ya taifa ya Ureno mbele ya  Ujerumani katika mashindano yoyote kwa miaka 25.

Ronaldo ambaye sasa ana umri wa miaka 40, pia ndiyo anaongoza kwa wachezaji waliofunga mabao mengi katika timu za taifa baada ya kufikisha miaka 30 na kuendelea.

Kiujumla tangu afikishe miaka 30, Ronaldo amefunga mabao 83 wakati mpinzani wake wa karibu Lionel Messi akiwa na mabao 54 katika nafasi ya pili ya orodha hiyo.

Vilevile Mreno huyu anaendelea kujichimbia kileleni katika rekodi yake ya kuwa na mabao mengi zaidi katika timu ya taifa ambapo kwa sasa anaongoza akiwa na mabao 137 huku Messi akiwa na 112.

Kwa sasa Ronaldo ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Al-Nassr  kumalizika mwisho wa msimu uliopita lakini mazungumzo juu ya mkataba mpya bado yanaendelea lakini hadi sasa bado hakuna mwafaka uliofikiwa.