Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Real Madrid yapata mkali mipira iliyokufa

Muktasari:

  • Kuondoka kwa wachezaji kama Cristiano Ronaldo, Gareth Bale, Sergio Ramos, Isco na Toni Kroos, miongoni mwa wengine kuliiacha Madrid bila chanzo cha uhakika cha hatari kupitia mipira iliyokufa, lakini sasa Guler anaonekana kuwa tayari kuziba pengo hilo kutokana na ubora wa mipira anayopiga na kuanza kuaminiwa kufanya hivyo na kocha Jose Mourinho.

ELDA, HISPANIA; BAADA ya miaka kadhaa ya kuhangaika kumpata mrithi wa wataalamu wake mahiri wa mipira ya adhabu (iliyokufa), kuibuka kwa Arda Güler kama mchezaji anayesimamia eneo hilo moja kwa moja kumeipa Real Madrid silaha mpya.

Kuondoka kwa wachezaji kama Cristiano Ronaldo, Gareth Bale, Sergio Ramos, Isco na Toni Kroos, miongoni mwa wengine kuliiacha Madrid bila chanzo cha uhakika cha hatari kupitia mipira iliyokufa, lakini sasa Guler anaonekana kuwa tayari kuziba pengo hilo kutokana na ubora wa mipira anayopiga na kuanza kuaminiwa kufanya hivyo na kocha Jose Mourinho.

Baada ya kuonyesha kiwango bora na kuwa miongoni mwa wachezaji bora wa Real Madrid katika mchezo dhidi ya Rayo Vallecano, Guler alirejea kwenye kikosi cha kwanza dhidi ya Elche. Dakika 25 tu baada ya mchezo kuanza, kiungo huyo wa kimataifa wa Uturuki aligonga vichwa vya habari kwa kupiga mpira mzuri wa adhabu ambao, kwa msaada wa kipa Matías Dituro uliingia wavuni na kuipa Madrid bao la kuongoza 1-0.

Bao hilo lilimaliza ukame mrefu zaidi wa Real Madrid wa kufunga kwa mpira wa adhabu ya moja kwa moja katika historia yake ya LaLiga; mechi 120 mfululizo za ligi bila kufunga bao kutokana na mpira wa adhabu ya moja kwa moja.

Ili kuipata bao la mwisho Real Madrid katika hali hiyo unatakiwa kurudi hadi katika siku ya 37 ya msimu wa 2022-23, wakati Rodrygo Goes alipofunga moja ya mabao yake mawili dhidi ya Sevilla kupitia mipira ya adhabu ya moja kwa moja.

Katika misimu minne iliyopita, ukiwamo huu,Real Madrid imefunga mabao manne pekee ya adhabu hizo kutokana na mipira ya kufa. Guler amehusika na mawili kati yake na, akiwa pamoja na Trent Alexander-Arnold ameibuka kuwa miongoni mwa wapigaji bora wa mipira ya adhabu katika timu hiyo. Cha kushangaza zaidi ni ukame wa Real Madrid kwenye uwanja wake wa nyumbani. Uwanja wa Bernabeu haujashuhudia bao la Real Madrid kutokana na mpira wa adhabu tangu ilipocheza dhidi ya Roma katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2018-19. Sasa Guler akiwa amepewa jukumu la kusimamia mipira hiyo, huenda ukame huo ukafikia mwisho.

Akizungumzia hilo, Mourinho aligoma kueleza iwapo tayari ameshaamua kuwa Guler ndiye mpigaji wa mipira iliyokufa moja kwa moja au la, lakini alisisitiza kwamba kuna kinachofanyika.

“Arda siyo lazima. Hakuna mtu aliye muhimu na wa lazima. Tulikuwa tunapoteza udhibiti nilipofanya mabadiliko. Vini alifanya kazi nzuri sana. Na Arda ni bora kwa sasa," alisema.