Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ratiba ngumu ya Mayweather yaahirisha pambano na Mike Tyson

Muktasari:

  • Mayweather ana ratiba yenye mapambano kadhaa yaliyopangwa mwaka huu, ikiwemo dhidi ya Manny Pacquiao.

NEW YORK, MAREKANI: PAMBANO la Floyd Mayweather Jr na Mike Tyson lililotarajiwa kufanyika mapema mwaka huu inadaiwa kuahirishwa kutokana na ratiba ngumu ya Mayweather kwa mwaka huu.

Mayweather ana ratiba yenye mapambano kadhaa yaliyopangwa mwaka huu, ikiwemo dhidi ya Manny Pacquiao.

Bondia huyo mwenye jina la utani la 'Money' anatarajiwa kupambana tena na Pacquiao kutokana na tangu mara ya mwisho wapigane katika pambano lao maarufu la mwaka 2015 lililopewa jina la Fight of the Century na hili litakuwa pambano lake la kwanza la kulipwa tangu mwaka 2017.

Pambano dhidi ya Pacquiao linatarajiwa kufanyika Septemba 19 katika Jiji la Las Vegas kwenye Ukumbi wa Sphere.

Mbali na hilo, Mayweather pia ana pambano la lingine lililopangwa kufanyika Juni dhidi ya mkongwe wa kickboxing kutoka Ugiriki Mike Zambidis.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za ndondi Dan Rafael, pambano la Tyson dhidi ya Mayweather “halitafanyika kabisa” katika tarehe iliyopangwa hapo awali ambayo ilikuwa ni April, 25.

Kutokana na mtandao wa X, Rafael aliandika: “Kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu pambano la kati ya Mike Tyson na Floyd Mayweather kufanyika Aprili 25 huko Dr Congo, lakini kwa mujibu wa chanzo kinachofahamu mipango hiyo, ni halitafanyika katika tarehe hiyo. Litaahirishwa hadi tarehe nyingine."

Kutokana na ratiba ya Mayweather kubana sana, inawezekana pambano hilo likapangiwa kufanyika Mei au Julai. Lakini ikiwa litacheleweshwa zaidi, kuna uwezekano likaahirishwa kabisa kwa sababu atalazimika kuanza maandalizi ya pambano lake dhidi ya Pacquiao mwezi Septemba.

Kwa upande wa Tyson, alikuwa akirejea mara kadhaa ulingoni katika miaka ya karibuni. Miongoni mwa mapambano yake makubwa ni lile la uzito wa juu dhidi ya Jake Paul, ambalo Paul alishinda pointi.