Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pirates kumuachia mfungaji wake

Muktasari:

  • Kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita, uongozi wa Pirates umekuwa kwenye mazungumzo na nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa lengo la kuongeza mkataba wake na kumbakisha ndani ya kikosi hicho.

PRETORIA,  Afrika Kusini: KLABU ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini inakabiliwa na uwezekano wa kumpoteza mshambuliaji wake tegemeo, Monnapule Saleng, kuelekea dirisha la usajili baada ya mazungumzo ya kuongeza mkataba wake kukwama.

Kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita, uongozi wa Pirates umekuwa kwenye mazungumzo na nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa lengo la kuongeza mkataba wake na kumbakisha ndani ya kikosi hicho.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa za Africasoccer.com, mazungumzo hayo yamekwama kutokana na madai ya mshahara ya mchezaji huyo ambayo uongozi wa klabu hiyo bado haujakubali.

Tangu alipojiunga na Pirates mwaka 2021, Saleng amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu katika kikosi hicho kutokana na mchango wake uwanjani.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kuna klabu tatu ambazo hazijatajwa majina zikionyesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Afrika Kusini katika dirisha lijalo la usajili.

Katika msimu huu, Saleng amecheza mechi 13 katika mashindano yote akiwa na Pirates, akifunga mabao matano na kutoa pasi mbili za mabao.

Kwa upande wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Saleng alicheza mchezo wake wa kwanza Juni 2021 na tangu wakati huo amecheza mechi 10 bila kufunga bao wala kutoa pasi ya bao.