Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Partey atua anga za Barcelona

TETESI Pict

Muktasari:

  • Partey ambaye anadaiwa pia kuwa katika mazungumzo ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia, msimu uliopita alicheza mechi 52 za michuano yote.

BARCELONA imeanza mazungumzo na kiungo wa Arsenal na Ghana, Thomas Partey, 31, kuhusu uhamisho wa bure katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo mkataba wake utamalizika.

Partey ambaye anadaiwa pia kuwa katika mazungumzo ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia, msimu uliopita alicheza mechi 52 za michuano yote.

Awali, staa huyo aliripotiwa kuwa huenda angerejea Atletico Madrid iliyokuwa ikihitaji kumsajili, lakini sasa mambo yanaonekana kubadilika.

Mpango wa Arsenal kutaka kumbakisha unaonekana kuibuka hivi karibuni baada ya kuonyesha kiwango bora katika nusu ya msimu uliopita.

Mojawapo kati ya sababu zilizotajwa zinaisukuma Arsenal kuachana naye ilikuwa ni hali yake ya majeraha ya mara kwa mara.

Pamoja na Barcelona na Arsenal, pia kuna timu kibao ambazo zinaonekana kumfuatilia mchezaji huyo zikiwamo za Ligi Kuu Saudi Arabia, ambako inadaiwa kwamba amewekewa dau nono akitua msimu ujao.

Tayari baadhi ya timu ikiwa Al Nassr na Al Ittihad zimekuwa katika maboresho ya vikosi kwa ajili ya msimu ujao na zimetenga mzigo wa maana kwa ajili ya kusajili nyota kadhaa kutoka Ulaya.


Milos Kerkez

LIVERPOOL inajiandaa kuwasilisha ofa rasmi kwenda Bournemouth ili kuipata saini ya beki wa kushoto wa Bourmeouth na timu ya taifa ya Hungary, Milos Kerkez, mwenye umri wa miaka 21, ambaye tayari amekubali uhamisho huo. Kwa sasa Liverpool inataka tu kumalizana na timu yake katika masuala ya ada ya uhamisho ambapo inatakiwa kutoa Pauni 40 milioni.


Florian Wirtz

OFA ya pili iliyowasilishwa na Liverpool kwenda Bayer Leverkusen kwa ajili ya kiungo  mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Ujerumani, Florian Wirtz, 22, imekataliwa na taarifa zinaeleza Liverpool inataka kuwajumuisha mastaa wake  Harvey Elliott, 22, na Jarell Quansah, 22, kama sehemu ya dili hilo pamoja na kiasi cha pesa.


Liam Delap

MSHAMBULIAJI wa Ipswich na timu ya taifa ya England, Liam Delap, 22, amekamilisha sehemu ya kwanza ya vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga na Chelsea kwa ada ya uhamisho ya Pauni 30 milioni. Delap ambaye msimu uliomalizika alicheza mechi 40 michuano yote na kufunga mabao 12 amezikataa timu mbalimbali na kuikubali Chelsea.


Matt O’Riley

EVERTON inaonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Brighton, Matt O’Riley, mwenye umri wa miaka 24, lakini haina uhakika kama timu yake itakuwa tayari kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark. Tangu kuanza kwa msimu uliopita amecheza mechi 29 za michuano yote na kufunga mabao mawili. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2029.


Viktor Gyokeres

MKURUGENZI wa michezo wa Barcelona, Deco de Souza amesema hawana mpango wa kusajili mshambuliaji mpya katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi licha ya kuhusishwa na straika wa Sporting Lisbon na timu ya taifa ya Sweden, Viktor Gyokeres, mwenye umri wa miaka 26, ambaye pia anawindwa na Arsenal na Manchester United.


Caoimhin Kelleher

BRENTFORD imekubali kulipa Pauni 12.5 milioni ili kuipata saini ya kipa wa Liverpool na timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland, Caoimhin Kelleher katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Mabosi wa Brentford wanataka kumsajili mchezaji huyo ili kuziba pengo la kipa raia wa Uholanzi anayetarajiwa kutua Bayer Leverkusen katika dirisha hilo mara tu litakapofunguliwa.


James Trafford

NEWCASTLE huenda ikalazimika kutoa dau kubwa ili kumsajili kipa wa Burnley na timu ya taifa ya England, James Trafford, mwenye umri wa miaka 22, kwani kocha Scott Parker hataki kuona supastaa huyo akiondoka kikosini akiamini atasaidia timu katika msimu ujao wa Ligi Kuu England ambapo wamepanda daraja. Mkataba wa sasa wa Trafford unatarajiwa kumalizika mara tu itakapofika 2027.