Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

No Yamal, no Salah, no Mayele... Kombe la Dunia litaleta bingwa wa kweli?

DUNIA Pict

Muktasari:

  • Mwezi Aprili mwaka huu, Rais wa FIFA Gianni Infantino alisimama kwenye jukwaa la Uwanja wa Rose Bowl huko Pasadena na kusifu mfumo mpya wa mashindano haya ambayo yatashirikisha timu 32 kutoka mabara yote.

NEW YORK, MAREKANI: IKIWA zimebakia siku mbili kabla ya mashindano ya Kombe la dunia la klabu kuanza huko Marekani, mjadala mkubwa umeibuka juu ya timu zilizofuzu na zile zilizoshindwa kufuzu michuano hiyo.

Mwezi Aprili mwaka huu, Rais wa FIFA Gianni Infantino alisimama kwenye jukwaa la Uwanja wa Rose Bowl huko Pasadena na kusifu mfumo mpya wa mashindano haya ambayo yatashirikisha timu 32 kutoka mabara yote.

Infantino  alidai kuwa Kombe hili la Dunia kwa Klabu litaamua, “kwa mara ya kwanza katika historia”, ni timu gani bora zaidi duniani.

Kauli ya michuano hiyo kuleta timu bora zaidi duniani wa sasa inaonekana kupingwa kwani kundi kubwa la timu zilizofanya vizuri msimu uliopita hazijapata nafasi ya kushiriki michuano hiyo.

Huu hapa ni uchambuzi juu ya timu bora zilizokwama kushiriki, sababu pamoja na timu ambazo zinaonekana kuwa na hali mbaya lakini zikapata nafasi ya kushiriki.

DUNI 05

PICHA KAMILI

Kabla ya mfumo huu mpya, hapo awali kufuzu michuano hii lilikuwa ni jambo gumu kwa sababu ilishirikisha mabingwa wa mwaka husika tu kutoka mabara yote.

Katika mfumo huu ambao kila bara limepewa nafasi ya kutoa wawakilishi waliokuwa mabingwa wa Ligi ya Mabingwa kuanzia mwaka 2021 hadi 2024, pia FIFA imetoa nafasi za ziada kwa mashirikisho ya mabara husika ambapo ilipelekea kuwa na mwakilishi mmoja kutoka OFC, wanne kutoka CAF, CONCACAF na AFC kila moja, sita kutoka CONMEBOL na 12 kutoka UEFA.

Kwa bahati mbaya, mchakato huu wa kufuzu umepelekea kuwepo kwa timu ambazo hazikutarajiwa kuwepo kwa sababu hazifanyi vizuri kwa sasa, pia kuwepo kwa timu ambazo zilitarajiwa kuwepo kwa kufanya kwao vizuri lakini hazipo.


WASHINDI WA 2025 HAWAPO

Ingawa ni jambo linaloeleweka kwamba washiriki walichaguliwa kulingana na mafanikio kwenye  bara lao kwa kipindi cha miaka minne iliyopita, muda huo unaonekana ni mwingi sana. Kwa mfano, Monterrey haijawahi kushinda taji lolote tangu waliposhinda Kombe la Mabingwa la CONCACAF mwaka 2021, na mwaka huu hawakuvuka robo fainali ya ligi ya Mexico (Liga MX).

Vilevile hata  Wydad AC, waliotwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2022, mwaka huu hawakufuzu kabisa kushiriki mashindano hayo.

Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, Pyramid ambao wanaonekana kufanya vizuri zaidi hawajapata nafasi ya kushiriki sawa na ilivyo kwa mabingwa wa CONCACAF (Cruz Azul) na AFC (Al-Ahli), jambo linalopunguza uhalali wa kauli ya Infantino kwamba timu 32 bora zaidi duniani ndio zinashiriki michuano hiyo.


KIAJABU HAWAPO

Kwa upande wa Ulaya, mambo ndiyo yanaonekana kushangaza zaidi, Bahati nzuri tu, PSG na Inter Milan waliofika fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya watakuwepo katika michuano hiyo kutokana na nafasi zao kwenye  viwango vya UEFA.

Hata hivyo, mabingwa wa Italia (Napoli) iliyokuwa ikiongozwa na wakali Romelu Lukaku na Scott McTominay,   huku kwa Ureno (Sporting CP) imezikosa ikiwa na nyota wake wanaotazamwa kwa sasa kama Viktor Gyokeres, Uhispania (Barcelona) na nyota wake Lamine Yamal  na England (Liverpool) ya Mohammed Salah. Fikiria wote hao hawatokuwepo.

Napoli wamechukua taji la Serie A mara mbili ndani ya misimu mitatu.

Sporting CP imetetea ubingwa wao wa Ureno na Barcelona ya Hansi Flick msimu huu imeshinda Supercopa de Espana, Copa del Rey na La Liga, huku wakiichapa  Real Madrid mara nne msimu huu.

DUNI 01

LIVERPOOL NJE, SALZBURG NDANI?

Liverpool, kwa upande wake, ilitawala Ligi Kuu ya England msimu huu na ilikuwa timu ya nane bora kwenye viwango vya UEFA wakati nafasi za kufuzu zikitolewa (sasa wako nafasi ya nne, nyuma ya Madrid, Man City na Bayern).

Lakini sheria ya kuzuia kila nchi kuwa na zaidi ya timu mbili (isipokuwa kwa vilabu kama kimoja kimeshinda taji la bara) iliwafanya Liverpool kukosa nafasi, huku Chelsea wakifuzu kutokana na ushindi wao wa Ligi ya Mabingwa mwaka 2021, japo hawajashiriki tena mashindano hayo kwa miaka miwili.

Sheria hiyo pia iliwazuia Napoli na Barca, na ikairuhusu Red Bull Salzburg kushiriki, japo si timu bora hata ndani ya Austria, na wapo nafasi ya 44 kwenye viwango vya UEFA.

DUNI 02

ISHU YA MESSI

FIFA, kama kawaida, ilihitaji timu kutoka nchi mwenyeji ambaye watu wengi walitarajiwa kuwa atachaguliwa mshindi wa MLS Cup 2024. Badala yake, nafasi hiyo ilipewa Inter Miami.

Hii ilionekana ni kama njama ya kuhakikisha Lionel Messi anashiriki mashindano hayo  na kauli ya Infantino kwamba timu moja miongoni mwa washiriki ilikuwa inataka kumsajili Cristiano Ronaldo ili kucheza kwenye mashindano haya, iliongeza mashaka zaidi.

Infantino alisema kuwa Inter Miami walistahili kwa sababu tayari walikuwa wameonyesha kuwa ni timu bora uwanjani licha ya  LA Galaxy ndio waliotwaa MLS Cup ikiwa ni mwezi mmoja baada ya Messi na Inter Miami yake  kutolewa mapema kwenye hatua ya mtoano.