Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nicolas Jackson aingia anga za Atletico

Muktasari:

  • Licha ya kuonyesha nia na kuwa tayari kutoa pesa ili kumsajili, taarifa zinadai Chelsea haina mpango wa kumuuza fundi huyu.

ATLETICO Madrid inataka kutuma ofa kwenda Chelsea katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kuipata saini ya mshambuliaji wa timu hiyo na Senegal, Nicolas Jackson, 23.

Licha ya kuonyesha nia na kuwa tayari kutoa pesa ili kumsajili, taarifa zinadai Chelsea haina mpango wa kumuuza fundi huyu.

Jackson ambaye msimu huu amecheza mechi 24 za michuano yote, akafunga mabao tisa na kutoa asisti tano, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2033.

Atletico inataka kumsajili Jackson kwa ajili ya kuboresha eneo lao la ushambuliaji ambalo kocha Diego Simeone anaona lina mapungufu kwa msimu huu.

Staa huyu kwa sasa yupo nje kutokana na majeraha aliyopata katika mchezo dhidi ya West Ham na anatarajiwa kurejea April Mosi, mwaka huu.


Ibrahima Konate

PARIS St-Germain wameonyesha nia ya kutaka kumsajili beki wa Liverpool na  Ufaransa, Ibrahima Konate, mwenye umri wa miaka 25, ambaye yuko tayari kujiunga na mabingwa hao wa Ligue 1. Konate ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha majogoo wa Jiji la Liverpool na msimu huu amecheza mechi 26 za michuano yote na kufunga mabao mawili.


Nicolas Kuhn

NEWCASTLE United imeingia katika vita dhidi ya Brentford na Brighton  kwa ajili ya kuipata saini ya  mshambuliaji wa Celtic na Ujerumani, Nicolas Kuhn, mwenye umri wa miaka 25. Kuhn ni miongoni mwa mastraika walioonyesha kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu ambapo amecheza mechi 35 za michuano yote na kufunnga mabao 17. Mkataba wake unamalizika 2029.


Florian Wirtz

MANCHESTER City inapambana vikali na  Bayern Munich katika mbio za kumsaini kiungo mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Ujerumani, Florian Wirtz, 21, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Wirtz amekuwa akihitajika na vigogo mbalimbali barani Ulaya tangu msimu uliopita alipoisaidia Leverkusen kuchukua ubingwa wa Bundesliga. Msimu huu amecheza mechi 34 za michuano yote na kufunga mabao 15.


Marc Casado

CHELSEA imeanza kuwasiliana na  wawakilishi wa kiungo wa Barcelona, Marc Casado, 21, ambaye amekuwa mhimili muhimu kwenye safu ya kiungo ya Barcelona.

Casado aliyepandishwa kutoka timu ya vijana ya Barca Julai mwaka jana, msimu huu amecheza mechi 30 za michuano yote. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2028.


Nico Williams

WINGA wa Athletic Bilbao na Hispania, Nico Williams, 22, anatamani zaidi kutua Barcelona licha ya uwepo wa timu nyingi kutoka England zinazohitaji saini yake kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Staa huyu tegemeo katika kikosi cha Bilbao, huduma yake inawindwa na Arsenal na Liverpool ambazo zipo tayari kulipa kiasi cha pesa kinachohitajika ili kumpata lakini changamoto imekuwa kwa Nico mwenyewe ambaye anahitaji zaidi kutua Barca.


Pablo Barrios

CHELSEA imefanya makubaliano na wawakilishi wa beki kisiki wa Atletico Madrid, Pablo Barrios ili kuipata saini yake katika dirisha lijalo la majira ya kuangazi. Tangu kuanza kwa msimu huu, Pablo amecheza mechi 24 za michuano yote na Chelsea inataka kulipa Pauni 58.3 milioni. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2028.


Alexis Saelemaekers

MABOSI wa AS Roma wamefikia patamu katika mazungumzo yao na wawakilishi wa kiungo wa AC Milan na Ubelgiji, Alexis Saelemaekers, 25, ili kumsainisha mkataba mpya. Alexis ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Roma, msimu huu amecheza mechi 20 za michuano yote. Mkataba wa sasa wa Alexis na Milan unatarajia kumalizika 2027.