Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namba 9 bora England hawa hapa

NAMBA 09 Pict

Muktasari:

  • Alexander Isak amehusika moja kwa moja kwenye mabao 29 kwenye ligi msimu huu, akifunga mara 23 na kuasisti mara sita. Yupo juu kwa mabao manne dhidi ya Erling Haaland aliyefunga 21 na kuasisti mara tatu.

LONDON, ENGLAND: NANI straika bora kwenye Ligi Kuu England kwa sasa?

Alexander Isak amehusika moja kwa moja kwenye mabao 29 kwenye ligi msimu huu, akifunga mara 23 na kuasisti mara sita. Yupo juu kwa mabao manne dhidi ya Erling Haaland aliyefunga 21 na kuasisti mara tatu.

Hata hivyo, Isak na Haaland wanakabiliana na upinzani mkali katika kupata mshindi kwenye vita ya straika bora wa msimu kwenye Ligi Kuu England.

Kutokana na hilo, nani ni Namba 9 bora kwa sasa? Kwa mujibu wa Squawka Score, hii hapa orodha ya mastraika watano ambao ni bora kabisa kwenye Ligi Kuu England kwa sasa kwa kuzingatia dakika walizocheza msimu huu, walau zinazoanzia 1620.

NAMB 01

5. Chris Wood

Klabu: Nottingham Forest

Squawka Score: 67%

Yawezekana amepungua kasi yake ya kufunga kwa sasa, lakini Chris Wood anabaki kuwa mmoja wa mastraika bora kwenye Ligi Kuu England msimu huu. Straika huyo wa Nottingham Forest amefunga mabao 20, ikiwa ni wastani wa kufunga bao 0.64 kwa dakika 90. Wood ana wastani wa asilimia 53.97 wa usahihi wa mashuti yake ndani ya uwanja. Amehusika kwenye mabao 23, mashuti ndani ya boksi 35, nafasi kubwa za mashambulizi 13, kushinda mipira ya juu 92, kurudisha mpira kwenye umiliki 10, kusababisha faulo 22 na amegusa mpira ndani ya boksi la wapinzani mara 100, akiasisti mara tatu.

NAMB 02

4. Jorgen Strand Larsen

Klabu: Wolves

Squawka Score: 68%

Ni wakati wa watu kutambua uwepo wa staa huyo wa Norway kwenye Ligi Kuu England. Jorgen Strand Larsen alijiunga na Wolves kwa mkopo kutoka Celta Vigo mwaka jana na kuonyesha kile ambacho anaweza kukifanya uwanjani. Strand Larsen ana wastani wa kufunga bao 0.47 kwa kila dakika 90 kwenye ligi msimu huu, huku akiwa na wastani wa asilimia 62.26 ya usahihi wa mashuti yake. Amehusika na mabao 15, amegusa mpira ndani ya boksi la wapinzani mara 111, amepiga mashuti ndani ya boksi mara 35, asisti mbili, kushinda mipira ya juu mara 66, akisababisha faulo 18 na amerudisha mpira kwenye himaya ya timu yake mara 10.

NAMB 03

3. Yoane Wissa

Klabu: Brentford

Squawka Score: 72%

Yoane Wissa sasa atakuwa kwenye rada za klabu nyingi kuhitaji saini yake kutokana na kile alichokifanya Brentford msimu huu. Na hilo linamfanya kuwa mmoja wa mastraika bora wa Ligi Kuu England. Staa huyo wa kimataifa wa DR Congo ana wastani wa mabao 0.59 kwa dakika 90, huku akiwa na wastani wa asilimia 21.18 wa uwezekano wa kutumbukiza mipira nyavuni. Amehusika katika mabao 21 katika dakika 2747, huku akigusa mpira kwenye boksi la upinzani mara 153, mashuti kwenye boksi la wapinzani 45, kutengeneza nafasi kubwa mara 16, asisti tatu, akisababisha faulo mara 49 na kushinda mipira ya juu mara 30.

NAMB 04

2. Erling Haaland

Klabu: Man City

Squawka Score: 77%

Ni kitu cha kushangaza kuona Erling Haaland hayupo kwenye namba moja. Staa huyo wa kimataifa wa Norway amefunga mabao 21 kwenye Ligi Kuu England msimu huu. Kwa dakika 2573 alizocheza, staa huyo amechangia mabao 24, akigusa mpira ndani ya boksi la wapinzani mara 192, mashuti ndani ya boksi 62, asisti tatu, kutengeneza nafasi kubwa 18, ameshinda mipira ya juu mara 52 na kusababisha faulo mara 12 huku akirudisha mpira kwenye umiliki wa timu yake mara 13. Ana wastani wa asilimia 56.31 ya usahihi wa mashuti yake na wastani wa kufunga bao 0.66 kwa dakika 90.

NAMB 05

1. Alexander Isak

Klabu: Newcastle

Squawka Score: 81%

Hakuna mchezaji mwingine kwenye Ligi Kuu England mwenye rekodi bora ya kufunga mabao kumzidi Alexander Isak, ambaye mwanzoni alionekana kupata shida baada ya kufunga mara moja tu katika mechi sita za kwanza. Staa huyo amecheza dakika 2679, amechangia mabao 29, akigusa mpira ndani ya boksi la wapinzani 208, akipiga mashuti ndani ya boksi la wapinzani mara 49, akiasisti mara sita, akitengeneza nafasi 34, akishinda mipira ya juu 27 na kusababisha faulo mara 14 na kurudisha mpira kwenye umiliki wa timu yake ikiwa kwenye eneo la kushambulia mara 18. Yupo kwenye mbio za kusaka Kiatu cha Dhahabu.