Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtiti Kombe la Dunia la Klabu ngoja tuone!

Muktasari:

  • Licha ya uwepo wa timu nyingi, kuna timu chache ambazo zinapewa nafasi ya kufanya makubwa zaidi kuliko nyingine kutokana na sababu kadhaa, ikiwemo ukubwa wao, mafanikio na historia yao katika michuano hii.

FLORIDA, MAREKANI: MICHUANO ya Kombe la Dunia kwa klabu mwaka huu itahusisha timu nyingi zaidi kwa mara ya kwanza ikiwa ni mfumo mpya wa mashindano hayo.

Licha ya uwepo wa timu nyingi, kuna timu chache ambazo zinapewa nafasi ya kufanya makubwa zaidi kuliko nyingine kutokana na sababu kadhaa, ikiwemo ukubwa wao, mafanikio na historia yao katika michuano hii.

Hata hivyo, katika zile ambazo hazipewi sana nafasi kuna uwezekano zikashangaza kwa kufanya vizuri kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Hizi hapa ni timu tano ambazo zimewahi kushangaza katika michuano hii, licha ya kutopewa nafasi kubwa wakati mashindano yanaanza.


RAJA CASABLANCA (MOROCCO) - 2013

Raja Casablanca ilishiriki mashindano ya FIFA Club World Cup mwaka 2013 kama wenyeji wa michuano iliyoandaliwa Morocco.

Hali ilikuwa tofauti kwa kuwa ilijiingiza kama timu ya mwaliko, si kama mabingwa wa Afrika, jambo lililowafanya wengi kuamini ingeondolewa mapema.

Lakini historia iliandikwa kwa njia tofauti.

Ilipata ushindi wa kwanza wa mabao 2-1 dhidi ya Auckland City ya New Zealand, kisha iliichapa CF Monterrey ya Mexico, timu iliyokuwa na rekodi nzuri katika mashindano ya CONCACAF.

Katika nusu fainali, ilikabiliana na Atletico Mineiro ya Brazil, timu iliyoongozwa na staa wa zamani wa soka, Ronaldinho. Hata hivyo, Raja ilishangaza wengi baada ya kushinda mabao 3-1, kisha ikaingia fainali.

Fainali dhidi ya Bayern Munich ilipoteza kwa mabao 2-0. Hata hivyo, iliweka historia ya kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufika fainali ya FIFA Club World Cup kama timu ya mwaliko, si kama bingwa wa bara.


TP MAZEMBE (DR CONGO) - 2010

Mwaka 2010, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliandika ukurasa mpya wa historia katika soka la dunia. Ilikuwa timu ya kwanza kutoka nje ya Bara la Ulaya na Amerika Kusini kufika fainali ya FIFA Club World Cup.

Ilianza safari kwa kuifunga Pachuca ya Mexico bao 1-0, kisha ilifanya jambo lisilotarajiwa kwa kuicharaza Internacional ya Brazil, mabingwa wa Amerika Kusini, kwa mabao 2-0 nusu fainali. Ushindi huu uliiweka kwenye ramani ya dunia kama timu hatari. Hata hivyo, ilipokea kichapo cha mabao 3-0 d dhidi ya Inter Milan ya Italia.


AL AIN FC (UAE) - 2018

Mwaka 2018, Al Ain FC iliingia katika mashindano haya kama mabingwa wa ligi ya UAE na wawakilishi wa mwenyeji wa mashindano. Ingawa wengi hawakuwatarajia kufanya vizuri, ilijibu kwa vitendo.

Katika mchezo wa kwanza ilitoka sare ya 3-3 na Team Wellington ya New Zealand na ikaenda kushinda mikwaju ya penalti 4-3.

Ilitumia hali yao ya uzoefu na uwanja wa nyumbani kuiondoa ES Tunis ya Tunisia, mabingwa wa Afrika.

Katika nusu fainali, iliwachapa mabingwa wa Amerika Kusini, River Plate ya Argentina, kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 2-2.

Fainali ilicheza na Real Madrid na licha ya kufungwa 4-1, ilionyesha kiwango bora.


KASHIMA ANTLERS (JAPAN) -2016

Kashima Antlers ilishiriki kama mabingwa wa Ligi Kuu ya Japan. Katika mashindano iliitoa Auckland City, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Atletico Nacional ya Colombia, ikionyesha umakini wa hali ya juu katika kila mechi.

Ilifikia fainali na kuikabili Real Madrid, mabingwa wa Ulaya. Katika mechi hiyo, iliongoza kwa mabao 2-1 hadi dakika za mwisho za mchezo, kabla ya Cristiano Ronaldo kuanza kuonyesha ustadi wake kwa kufunga hat-trick na kuipa Real ushindi wa mabao 4-2.

Kupitia mechi hii baadhi ya mastaa walipata nafasi ya kusajiliwa barani Ulaya kutokana na viwango vyao. Mmoja kati ya mastaa hao ni Gaku Shibasaki aliyesajiliwa na CD Tenerife ya Hispania mwaka 2017.


AL ITTIHAD (SAUDI ARABIA) -2005

Katika mashindano ya mwaka 2005, Al Ittihad ilionyesha ushindani mkali sana licha ya kwamba ilikuwa ni mara yao ya kwanza kushiriki.

Ilianza kwa kushinda Al Ahly ya Misri kwa bao 1-0. Baada ya hapo ilicheza nusu fainali dhidi ya Sao Paulo ya Brazil na kupoteza kwa mabao 3-2, lakini ilionyesha kiwango bora sana. Ingawa haikufikia fainali, Al Ittihad ilitajwa sana.