Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MKWANJA: Masupastaa 10 wenye thamani kubwa zaidi sokoni kwa sasa

MKWANJA Pict

Muktasari:

  • Kwenye nafasi ya 10 katika orodha hiyo, anapatikana mchezaji mwenye umri mkubwa kuliko wote katika orodha yenyewe, ambaye ni Federico Valverde.

MADRID, HISPANIA: MASUPASTAA wa soka wenye thamani kubwa zaidi duniani wamewekwa hadharani, huku Ligi Kuu England ikiingiza mastaa wawili tu kwenye orodha hiyo.

Hilo limekuja kwenye kipindi hiki cha usajili, ambapo bahati ya dirisha hili la majira ya kiangazi lina awamu mbili, ambapo ya kwanza iliyokomea Juni 10 ilikuwa inatoa nafasi kwa timu zinazoshiriki fainali za Kombe la Dunia la Klabu kufanya usajili wa kuboresha vikosi vyao, wakati lile jingine litafunguliwa Juni 16 na kufungwa Septemba 1.

Na kwa klabu ambazo zitakuwa bize kufanya usajili kwenye dirisha hili, zinapaswa kufahamu thamani za wanasoka huko sokoni zinavyosoma, ambako mtandao wa Transfermarkt umeweka hadharani masupastaa 10, ambao ukihitaji saini zao itakulazimu ujipange kwelikweli kuvunja benki.

Kwenye nafasi ya 10 katika orodha hiyo, anapatikana mchezaji mwenye umri mkubwa kuliko wote katika orodha yenyewe, ambaye ni Federico Valverde.

Staa huyo wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 26, ametajwa kuwa na thamani ya Pauni 110 milioni kwa mujibu wa mtandao huo, hivyo ukihitaji saini yake itakulazimu kujipanga kihivyo.

Kiungo huyo ni mmoja wa wachezaji wanne wa Real Madrid waliotajwa kwenye orodha hiyo.

Kuna masupastaa watatu ambao thamani zao sokoni zinalingana, Pauni 118 milioni kutoka nafasi ya tisa hadi saba, huku kinachovutia wote umri wao unalingana, miaka 22.

Mastaa wa Kijerumani, Jamal Musiala na Florian Wirtz wanaocheza soka lao kwenye Bundesliga wanatumikia klabu za Bayern Munich na Bayer Leverkusen mtawalia, wakati staa wa Hispania, Pedri anakipiga katika kikosi cha Barcelona kinachoshiriki mikikimikiki ya La Liga.

Thamani ya Pedri imepanda kutoka Pauni 101 milioni baada ya ile orodha ya Machi mwaka huu, bila shaka hilo limechangiwa na kiwango chake bora alichokionyesha kwenye timu yake ambayo imeshinda taji la LaLiga msimu huu na kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo, kwenye orodha hiyo ya wakali watatu, Wirtz pekee ndiye anayehusishwa na uhamisho wa pesa nyingi kutoka kwenye klabu yake baada ya Liverpool kupambana kumng’oa Bayer ili akakipige Anfield.

Liverpool hivi karibuni iliweka mezani ofa ya Pauni 113 milioni, huku Bayer ikihitaji walau kulipwa Pauni 126 milioni kwenye mauzo ya kiungo mshambuliaji huyo ili ipatikane pesa ya kumpa Erik ten Hag asajili wabadala wake. Mchezaji namba sita kwenye orodha hiyo ya wenye thamani kubwa sokoni ni staa wa Arsenal, Bukayo Saka, anayetajwa kuwa na thamani ya Pauni 126 milioni.

Uwezo wa Saka, 23, unajieleza wazi kutokana na kile ambacho amekuwa akifanya uwanjani, hashikiki.

Kwenye tano bora, supastaa wa Kibrazili, Vinicius Jr, ambaye huko nyuma alikuwa kwenye nafasi za juu kabisa akiwa na thamani ya Pauni 169 milioni, sasa ameporomoka kutokana na kiwango chake kuzorota huko Real Madrid, ambako kwa sasa anathaminishwa kwa Pauni 143 milioni.

Na juu yake yupo mchezaji mwenzake wa Los Blancos, Kylian Mbappe, ambaye licha ya kutoshinda taji lolote msimu huu, thamani yake imepanda na kufikia Pauni 152 milioni.

Thamani kama hiyo pia inawahusu pia mastaa wa zamani wa Borussia Dortmund, Erling Haaland na Jude Bellingham. Straika wa Manchester City, Haaland, 24, huko nyuma alikuwa na thamani ya Pauni 169 milioni, lakini kama ilivyo kwa Vinicius, kiwango chake uwanjani kumeshuka na baada ya timu yake kushindwa kubeba taji lolote na thamani yake sokoni imeporomoka.

Bellingham, 21, alinusurika na sakata la kushuka thamani yake, akibaki kwenye Pauni 152 milioni.

Hata hivyo, thamani ya mastaa hao watatu wote wapo nyuma ya mkali wa Barcelona, Lamine Yamal.

Yamal, ambaye anapewa nafasi kubwa ya kunyakua Ballon d’Or mwaka huu kutokana na kiwango chake matata uwanjani, ndiye mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi sokoni, Pauni 169 milioni, ikiwa ikiwa na maana kwamba ndiye mwanasoka ghali zaidi duniani.

Yamal alisaini mkataba wake mpya huko Barcelona hivi karibuni, unaomshuhudia akilipwa Pauni 33.5 milioni kwa mwaka. Staa wa Chelsea, Cole Palmer ameshidwa kidogo kuingia kwenye 10 bora baada ya kuwa na thamani ya Pauni 102 milioni, sawa na ilivyo kwa kiungo wa Arsenal, Declan Rice na straika wa Newcastle United, Alexander Isak.

Staa wa zamani wa Crystal Palace, Michael Olise ndiye anayeshika namba 20, ambapo thamani yake ni Pauni 85 milioni kutokana na kile alichofanya huko Bayern Munich. Hiyo inafanana na Alexis Mac Allister na Phil Foden, ambapo staa wa Man City na England, Foden thamani yake imeshuka kwa Pauni 25 milioni.

Washindi wa medali za ubingwa za Ligi ya Mabingwa Ulaya, Desire Doue na Khvicha Kvaratskhelia thamani zao zimepanda na kufikia Pauni 76 milioni, sawa na ilivyo kwa mkali mwingine anayepewa nafasi kubwa ya kushinda Ballon d’Or mwaka huu, Ousmane Dembele.