Mishahara ya Man United Amad akibamba dili jipya
Muktasari:
- Winga huyo, 22, amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na nusu, jambo litakalomfanya kubaki Old Trafford hadi Juni 2030.
MANCHESTER, ENGLAND: AMAD Diallo mambo yake ni safi baada ya kupandishiwa mshahara kufuatia dili jipya alilosaini Man United.
Winga huyo, 22, amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na nusu, jambo litakalomfanya kubaki Old Trafford hadi Juni 2030.
Na sasa, Amad atakuwa analipwa Pauni 100,000 kwa wiki, ikiwa ni mara tatu ya kiwango alichokuwa akilipwa kwenye mkataba uliopita.
Baada ya dili hilo, Amad alisema: “Najivunia sana kusaini huu mkataba mpya. Nilikuwa na nyakati nzuri kwenye hii klabu, lakini kuna mambo mengi zaidi mazuri yanakuja. Nina matamanio makubwa na huu mchezo na nataka kufikia mafanikio ya kihistoria hapa Man United.
“Nimejifunza mengi tangu nilipotua hapa miaka minne iliyopita. Nawashukuru makocha na wafanyakazi wengine ambao wamesaidia kunikuza na mashabiki wanaonipa hamasa ya kusonga mbele kila siku... ”
Dili hilo jipya la Amad linamfanya kupanda nafasi za juu kwenye wakali wanaolipwa mishahara mikubwa Man United akiwapiku mastaa kama Rasmus Hojlund, Alejandro Garnacho na Diogo Dalot. Wakati huo, kiungo Kobbie Mainoo, ambaye ni zao la kutoka kwenye akademia ya timu hiyo, ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mdogo zaidi kuliko wote. Casemiro ndiye anayeongoza kwa mshahara, analipwa Pauni 375,000 kwa wiki.
Anafuatiwa na Marcus Rashford na nahodha Bruno Fernandes kila mmoja analipwa Pauni 325,000 kwa wiki. Man United imeripotiwa kuwa na mpango wa kumwondoa Rashford kwenye bili yao ya mishahara mwaka huu kutokana na kiwango chake kibovu. AC Milan, Tottenham Hotspur na Arsenal zinaripotiwa kuhitaji huduma ya fowadi huyo Mwingereza.
Mason Mount - ambaye amecheza mechi 32 tu tangu alipojiunga na Man United, Julai 2023 - anashika namba nne kwa mshahara, akilipwa Pauni 250,000 kwa wiki, huku Antony - mchezaji aliyesajiliwa kwa Pauni 86 milioni karibu miaka mitatu iliyopita, analipwa Pauni 200,000 kwa wiki. Baada ya hapo, wanafuatia Matthijs de Ligt, Harry Maguire na Christian Eriksen. Lisandro Martinez, Victor Lindelof, Andre Onana na Leny Yoro ni wachezaji wengine wenye mishahara ya kati sawa na wakali wengine wawili waliosajiliwa kwenye dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana, Noussair Mazraoui na Manuel Ugarte.
MISHAHARA YA MAN UNITED KWA MSIMU WA 2024-25
-Casemiro, Pauni 375,000 kwa wiki
-Bruno Fernandes, Pauni 325,000 kwa wiki
-Marcus Rashford, Pauni 325,000 kwa wiki
-Mason Mount, Pauni 250,000 kwa wiki
-Antony, Pauni 200,000 kwa wiki
-Mathijs De Ligt, Pauni 195,000 kwa wiki
-Harry Maguire, Pauni 190,000 kwa wiki
-Christian Eriksen, Pauni 150,000 kwa wiki
-Luke Shaw, Pauni 150,000 kwa wiki
-Noussair Mazraoui, Pauni 135,000 kwa wiki
-Manuel Ugarte, Pauni 120,000 kwa wiki
-Victor Lindelof, Pauni 120,000 kwa wiki
-Lisandro Martinez, Pauni 120,000 kwa wiki
-Andre Onana, Pauni 120,000 kwa wiki
-Leny Yoro, Pauni 115,000 kwa wiki
-Joshua Zirkzee, Pauni 105,000 kwa wiki
-Amad Diallo, Pauni 100,000 kwa wiki
-Diogo Dalot, Pauni 85,000 kwa wiki
-Rasmus Hojlund, Pauni 85,000 kwa wiki
-Tyrell Malacia, Pauni 75,000 kwa wiki
-Jonny Evans, Pauni 65,000 kwa wiki
-Alejandro Garnacho, Pauni 50,000 kwa wiki
-Tom Heaton, Pauni 45,000 kwa wiki
-Altay Bayindir, Pauni 35,000 kwa wiki
-Kobbie Mainoo, Pauni 20,000 kwa wiki