Mgawo wa mkwanja kwa timu zote Europa League msimu huu

Muktasari:
- Timu hizo zilizitupa nje Bodo/Glimt na Athletic Bilbao kwenye nusu fainali mtawalia, lakini vijana wa kocha Ange Postecoglou ndio walioibuka na ushindi katika fainali hiyo iliyofanyika Bilbao, Hispania.
LONDON, ENGLAND: NI rasmi, Tottenham Hotspur imefuta ukame wake wa mataji uliodumu kwa miaka 17 baada ya kuichapa Manchester United 1-0 kwenye fainali ya Europa League msimu huu na kubeba ubingwa.
Timu hizo zilizitupa nje Bodo/Glimt na Athletic Bilbao kwenye nusu fainali mtawalia, lakini vijana wa kocha Ange Postecoglou ndio walioibuka na ushindi katika fainali hiyo iliyofanyika Bilbao, Hispania.
Kwa Man United, ingeshinda hilo lingempa nafasi kocha Ruben Amorim kubeba taji lake la kwanza Old Trafford. Lakini, kwa upande wa Spurs, ushindi huo umeifanya kubeba taji la kwanza kubwa kwa karibu miongo miwili.
Lakini, iwe timu imeshinda ubingwa au haijashinda, timu hizo mbili zote zimeweka kibindoni mkwanja wa maana baada ya kufika fainali iliyopigwa Jumatano iliyopita, Machi 21. Je, ni pesa kiasi gani timu hizo zimevuna?
Kwa mujibu wa Football Meets Data, hiki ndicho kiwango cha pesa kilichovunwa na timu zote 36 zilizoshindana kwenye mikikimikiki ya Europa League msimu huu.
Mgawo wa 36 - 27
Licha ya kuvuna pointi nyingi kwenye hatua ya League Phase, FC RFS ndiyo timu iliyopata mgawo mdogo wa pesa kwenye michuano hiyo msimu huu. Timu hiyo imevuna Pauni 5.3 milioni. OGC Nice, Maccabi Tel-Aviv na Union Saint-Gilloise ni timu nyingine zilizopo kwenye kundi hili.
Mgawo ulivyo;
27. RSC Anderlecht (Pauni 9.6milioni)
28. FC Twente (Pauni 9.2milioni)
29. Besiktas (Pauni 9.1milioni)
30. Union Saint-Gilloise (Pauni 8.1milioni)
32. Maccabi Tel-Aviv (Pauni 7.9milioni)
33. OGC Nice (Pauni 7.4milioni)
34. IF Elfsborg (Pauni 7milioni)
35. Ludogorets (Pauni 7milioni)
36. FC RFS (Pauni 5.3milioni)
Mgawo wa 26- 17
Baada ya kupenya kwenye League Phase, Jose Mourinho na chama lake la Fenerbahce ilitolewa mapema, lakini bado ilifanikiwa kuweka kibindoni Pauni 13.6 milioni. Kwenye kundi hilo kuna timu nyingine za FC Midtjylland, iliyovuna Pauni 13.4 milioni, wakati Viktoria Plzen, Braga na PAOK miongoni mwa timu zilizopo katika mgawo wa kundi hili.
Mgawo ulivyo;
17. Fenerbahce (Pauni 13.6milioni)
18. FC Midtjylland (Pauni 13.4milioni)
19. Viktoria Plzen (Pauni 12.5milioni)
20. Braga (Pauni 11.8milioni)
21. PAOK (Pauni 11.6milioni)
22. Dynamo Kyiv (Pauni 11.02milioni)
23. Malmo FF (Pauni 10.9milioni)
24. FC Steaua Bucharaest (Pauni 10.7milioni)
25. Hoffenheim (Pauni 10.6milioni)
26. Ferencvarosi (Pauni 10.5milioni)
26. Qarabag (Pauni 10.4milioni)
Mgawo wa 16 - 7
Baada ya kuonyeshana kazi na Manchester United kwenye robo fainali, Lyon ilitupwa nje kwenye michuano ya Europa League, lakini bado iliweka kibindoni mkwanja wa Pauni 19.3 milioni. Chini yake kuna timu kama Rangers, Roma na Ajax, ambazo pia zimevuna mkwanja wa kutosha kwenye mgawo uliotokana na michuano ya ya Europa League.
Mgawo ulivyo;
7. Lyon (Pauni 19.3milioni)
8. Rangers (Pauni 17.7milioni)
9. AS Roma (Pauni 17.6milioni)
10 .Ajax (Pauni 17.4milioni)
11. Olympiacos (Pauni 16.6milioni)
12. Real Sociedad (Pauni 16.1milioni)
13. Galatasaray (Pauni 15.7milioni)
14. AZ Alkmaar (Pauni 14.7milioni)
15. Slavia Prague (Pauni 14.3milioni)
16. Porto (Pauni 14.1milioni)
Mgawo wa 6 - 1
Man United imevuna Pauni 30.7 milioni kwenye mgawo wake, wakati Tottenham imevuna Pauni 38.2 milioni baada ya timu hizo mbili kufika hatua ya fainali. Timu za Athletic Bilbao na Bodo/Gimt nazo zilivuna pesa nzuri katika mgawo wa msimu huu kwenye mikikimikiki hiyo ya Europa League iliyohitimishwa uwanjani San Mames.
Mgawo ulivyo;
1. Tottenham Hotspur (Pauni 38.2milioni)
2. Manchester United (Pauni 30.7milioni)
3. FK Bodo/Glimt (Pauni 22.4milioni)
4. Lazio (Pauni 20.7milioni)
5. Athletic Club (Pauni 20.5milioni)
6. Eintracht Frankfurt (Pauni 20.5milioni)