Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mateta aliyeitungua Man United atakiwa Atletico

Tetesi Pict

Muktasari:

  • Crystal Palace inadaiwa kuwa tayari kumuuza, lakini kwa timu itakayokuwa tayari kulipa kiasi cha Pauni 50 milioni kama ada yake ya uhamisho.

ATLETICO Madrid ni miongoni mwa timu kubwa zinazohitaji saini ya straika wa Crystal Palace, Mfaransa Jean-Philippe Mateta, 27, ambaye mkataba wake na timu anayoichezea unatarajiwa kumalizika 2026.

Crystal Palace inadaiwa kuwa tayari kumuuza, lakini kwa timu itakayokuwa tayari kulipa kiasi cha Pauni 50 milioni kama ada yake ya uhamisho.

Mbali ya Atletico Madrid, pia Mateta anahitajika na Olympique Lyon.

Mchezaji huyo ambaye msimu huu amefunga mabao 13 katika mechi 28 alizocheza ametajwa sana baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa Ligi Kuu England ulioikutanisha Crystal Palace na Manchester United.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika ifikapo 2026, na timu yake ipo tayari kumuuza kwa sababu amekataa kusaini mkataba mpya ikiwa inahofia kwamba anaweza kuondoka bure.

Mchezaji huyo pia amekuwa akitakiwa na timu mbalimbali za Saudi Arabia.


Diogo Jota

ARSENAL inataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na Ureno, Diogo Jota, baada ya kuonekana hana nafasi ya kutosha katika kikosi cha Majogoo wa Anfield. Jota ambaye amekuwa akisumbuliwa sana na majeraha ya mara kwa mara, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika itakapofika 2027 na katika msimu huu amecheza mechi 21 za michuano yote na kufunga mabao manane.


Moise Kean

ARSENAL and Tottenham Hotspur zimeanza harakati za chinichini kwa ajili ya kumsajili straika wa Fiorentina na Italia, Moise Kean, 24, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kuboresha safu ya ushambuliaji inayoonekana kuwa na changamoto msimu huu. Kean ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2029, msimu huu amecheza mechi 28 za michuano yote na kufunga mabao 19.


Joao Felix

BARCELONA ilikataa ofa ya Chelsea iliyoipa nafasi ya kumsajili mshambuliaji raia wa Ureno, Joao Felix, 25, katika dirisha lililopita la majira ya baridi. Felix ambaye alitimkia kwa mkopo AC Milan baada ya dili lake la kwenda huko kufeli, anaonekana kuonyesha kiwango bora tangu atue katika kikosi hicho. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2031.


Fermin Lopez

MANCHESTER United na Aston Villa zilikuwa tayari kulipa Euro 70 milioni kwenda Barcelona ili kumsajili mshambuliaji Mhispania Fermin Lopez, 21, katika dirisha lililopita la majira ya baridi, lakini staa huyo aligoma kuondoka. Lopez ni mmoja wa mastaa walioonyesha viwango bora tangu kuanza kwa msimu huu akicheza mechi 25 za michuano yote na kufunga mabao matano.


Sandro Tonali

WAKALA wa kiungo wa Newcastle United, Sandro Tonali amesisitiza staa huyo hatarudi Italia kwa sasa licha ya tetesi zinazodai kuhusishwa na timu mbalimbali za nchi hiyo. Tonali ni mmoja kati ya wachezaji tegemeo Newcastle na msimu huu amecheza mechi 29 za michuano yote akifunga mabao matatu na kutoa asisti mbili. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2028.


Marc Guehi

BAADA ya kuona kuna uwezekano beki wa kati, Marc Guehi akaondoka dirisha lijalo la kiangazi, Crystal Palace imeanza kutafuta mbadala wake na miongoni mwa iliowaweka katika rada ni beki wa Burnley na Ufaransa Maxime Esteve, 22, na wa  Middlesbrough, Mholanzi Rav van den Berg, 20, ambao bado inawafuatilia.


Jamie Gittens

BORUSSIA Dortmund ipo tayari kumuuza winga raia wa England, Jamie Gittens, 20, anayewindwa na Liverpool, Manchester United na Chelsea dirisha lijalo. Uwezekano wa Gittens kuuzwa unadaiwa kuwa mkubwa ikiwa Dortmund itashindwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Mkataba wa staa huyo unatarajiwa kumalizika 2028.