Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa West Ham wamsapoti Antonio

Muktasari:

  • Mastaa hao wa West Ham United wote walivaa jezi yenye jina la Antonio yenye namba 9 mgongoni katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Wolves uliopigwa usiku wa juzi Jumatatu kwenye Uwanja wa London. Mechi hiyo ilimalizika kwa West Ham kushinda mabao 2-1.

LONDON, ENGLAND: WACHEZAJI wa West Ham United wameungana kumsapoti mchezaji mwenzao, Michail Antonio baada ya kupata ajali mbaya ya gari.

Mastaa hao wa West Ham United wote walivaa jezi yenye jina la Antonio yenye namba 9 mgongoni katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Wolves uliopigwa usiku wa juzi Jumatatu kwenye Uwanja wa London. Mechi hiyo ilimalizika kwa West Ham kushinda mabao 2-1.

Straika Antonio alipata ajali ya gari Jumamosi, ambapo mkali huyo mwenye umri wa miaka 34 alinusurika kifo baada ya gari yake ya Ferrari FF yenye thamani ya Pauni 260,000 kugonga mti huko Theydon Bois, Essex.

Antonio alinasa kwenye gari hilo kwa karibu saa moja kabla ya waokoaji kuja kukata gari kumtoa na kumpeleka hospitali kwa usafiri wa helikopta. Staa huyo wa kimataifa wa Jamaica aliumia mguu na kulazimika kufanyiwa upasuaji wa haraka kwenye hospitali moja huko London.

Tukio hilo liliibua taharuki kubwa kwenye Ligi Kuu England hasa katika klabu yake ya West Ham United.

Hata mashabiki waliohudhuria mechi hiyo alimsapoti straika wao baada ya kunyanyuka na kupiga makofi kwenye dakika ya tisa ya mchezo, wakimtakia kinara wao huyo wa mabao kwenye kikosi hicho kupona haraka na kurejea uwanjani.

Mchezaji Tomas Soucek naye alikuwa na kitu cha kufanya kuhusu Antonio baada ya kufunga kwa kichwa dakika ya 54 na kisha kushangilia kwa staili ya kuonyesha vidole tisa. Jarrod Bowen, ndiye aliyefunga bao la ushindi kwa West Ham na kisha kushangilia kwa kushika jezi ya Antonio baada ya Matt Doherty wa Wolves kusawazisha lile lililofungwa na Soucek katika mchezo huo uliokuwa wa vuta nikuvute.