Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man Uniuted yatua kwa Valverde

VALVEDE Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa Man United imepata nguvu zaidi ya kuamini kuwa inaweza ikampata staa huyo kutokana na hali ya kutoelewana kati yake na kocha wa timu hiyo Xabi Alonso.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United ipo kwenye mstari wa mbele ikifanya mazungumzo na wakala wa nyota wa Real Madrid, Federico Valverde ili kumsajili katika dirisha lijalo.

Inaelezwa Man United imepata nguvu zaidi ya kuamini kuwa inaweza ikampata staa huyo kutokana na hali ya kutoelewana kati yake na kocha wa timu hiyo Xabi Alonso.

Valverde ni miongoni mwa wachezaji kadhaa wa Madrid wanaodaiwa kutoridhishwa na mtindo wa uongozi wa Alonso na anataka kuondoka kwa sababu haoni kama kocha huyo anamthamini.

Kocha wa Man United, Ruben Amorim ni shabiki mkubwa wa Valverde na anatamani sana kuona fundi huyo akitua katika kikosi chake.

Hata hivyo, kiasi cha pesa kinachohitajika na Madrid kwa ajili ya kumuuza fundi huyo ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2029 kinatajwa kuwa ni Pauni 100 milioni.

Man United inaona kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 thamani yake haizidi Pauni 70 milioni, hivyo haipo tayari kutoa zaidi ya hapo.

Mbali ya Valverde, Alonso pia anatajwa kutokuwa katika uhusiano mzuri na staa mwingine wa timu hiyo Vinicius Jr jambo linalotishia uwezekano wa kuwa naye kwa msimu ujao kwani mchakato wa kumsainisha mkataba mpya unazidi kuwa mkubwa.

Man United inatajwa kuhitaji kiungo tangu dirisha lililopita, lakini ilifeli kufanikisha mchakato huo na sasa kumekuwa na majina ya viungo kadhaa wanaotajwa ikiwamo Carlos Baleba kutoka Brighton, lakini endapo Valverde atapatikana kwa bei inayowaridhisha wanaweza kuhamia kwake kutokana na uzoefu wake.